BRUCELLA
• • • • •
UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)
Huu ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama brucellosis na chanzo chake ni bacteria wanaojulikana kwa jina la Brucella,
bacteria hawa hutokea kwa wanyama, hivo ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
BACTERIA HAWA UNAWAPATA WAPI?
Bacteria hawa hutoka kwa wanyama mbali mbali kama vile; Ng'ombe, mbuzi,kondoo,Nguruwe,Mbwa n.k,
na kwa hivi sasa watu wengi hupatwa na ugonjwa wa Brucella ambao hupimwa kupitia kipimo cha damu,
Unaweza kupata bacteria hawa wa Brucella kwa kula nyama ambazo hazijapikwa vizuri au Maziwa
CHANZO CHA UGONJWA WA BRUCELLA
Hivo chanzo cha ugonjwa wa brucellosis ni bacteria wanaojulikana kwa jina la brucella, ambao husambaa kutoka kwa wanyama mbalimbali kama vile Ng'ombe na kwenda kwa binadamu
•Soma: Ugonjwa wa Wengu,Chanzo,Dalili pamoja na Matibabu yake
Dalili za Ugonjwa wa brucella
1. Mgonjwa kupatwa na homa ambazo hujirudia mara kwa mara
2. Mgonjwa kuhisi kama vile kuna vitu vinatembea mwilini mwake, na wakati mwingine huhisi kama minyoo wakati wa kujisaidia haja kubwa
3. Mgonjwa kuanza kutetemeka mwili baada ya kuhisi baridi kali
4. Mgonjwa kupoteza kabsa hamu ya kula chakula au kitu chochote
5. Mgonjwa kutoa jasho kupita kiasi
6. Mwili kuchoka sana pamoja na kuwa dhaifu
7. Mgonjwa Kupata maumivu ya joints,misuli pamoja na maumivu ya mgongo
8. Mgonjwa Kupata maumivu ya kichwa mara kwa mara
9. Pia mgonjwa huweza kupatwa na tatizo la kuvimba kwa kuta za ndani ya chemba za moyo yaani endocarditis
10. Mgonjwa kupatwa na tatizo la kuvimba kwa joints pamoja na mifupa ya uti wa mgongo yaani spinal bones, tatizo ambalo hujulikana kwa kitaalam kama Spondylitis.
DALILI ZINGINE ZA UGONJWA WA BRUCELLA NI PAMOJA NA;
- Mtu kuhisi hali ya vitu kutembea mwilini mwake
- Joto la mwili la mgonjwa kupanda au mgonjwa kuwa na homa
- Mgonjwa kupata maumivu makali ya mgongo
- Mgonjwa kuhisi hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika
- Kupata maumivu ya joint,misuli pamoja na viungo vya mwili
- Mgonjwa kuhisi uchovu wa mwili usio wa kawaida
- Uzito wa mwili kupungua kwa mgonjwa
- Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa
- Mgonjwa kupatwa na hali ya kutoa jasho jingi mwilini wakati wa usku
- Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya chakula
- Mgonjwa kupatwa na kikohozi cha mara kwa mara
- Mgonjwa kuumwa na tumbo
- Mgonjwa kupata rashes kwenye ngozi yake ya mwili
- Mwili kuwa dhaifu sana pamoja na kukosa nguvu
VIPIMO VYA UGONJWA WA BRUCELLA
Kulingana na hali ya mgonjwa pamoja na dalili ambazo zinajitokeza kwake,
Mambo mbali mbali huweza kufanyika kama hatua ya kwanza kabsa ili kufahamu chanzo halisi cha Ugonjwa wako,
mambo hayo ni Pamoja na;
- Mgonjwa kuelezea historia ya ugonjwa wake jinsi ulivyoanza(Patient history taking)
- Kufanya vipimo mbali mbali ikiwemo,
- Kipimo cha Damu(Blood tests)
- Kuchek Joto la Mwili
- Kupima presha(blood pressure)
- Uzito wa mgonjwa(body weight)
- Sukari n.k
MATIBABU YA UGONJWA WA BRUCELLA
Zipo dawa mbali mbali ambazo hutumika kutibu ugonjwa huu wa brucellosis na Ukaisha kabsa.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584
NAMNA YA KUJIKINGA NA BRUCELLA
Mpaka sasa hakuna chanjo ya BRUCELLA ilopatikana na kwa maana hiyo ni lazima kujilinda kwa njia zingine mpaka pale chanjo itakapopatikana..
1) Epuka kunywa maziwa mabichi; maziwa yanatakiwa yachemshwe kikamilifu
2) Epuka migusano ya majimaji ya wanyama tajwa na wewe, majimaji kama mate,uharo,mkojo,kondo la nyuma,kamasi nk.
3) Kuwapatia chanjo wanyama wote wafugwao au wanaokua karibu na binadamu dhidi ya chanjo ya brusela
4) Kwa wale wachinjaji na wauza nyama mabuchani wazingatie utaratibu Wa kazi zao ili kujilinda na migusano ya damu au majimaji yeyote kutoka kwa mnyama husika.
5) kwa zile jamii zilizo kwenye hatari ni vyema mkawa na desturi ya kupima homa ya brusela kwani unaeza kuambukuzwa brusela mwezi Wa kwanza lakini ukaja kuona dalili mwezi Wa 12.
Wanyama ambao unaweza kupata Brucella
Brucellosis huathiri wanyama wengi wa porini na wa nyumbani, Hii ni pamoja na:
- Ng'ombe
- Mbuzi
- Kondoo
- Nguruwe na nguruwe mwitu
- Mbwa, hasa wale wanaotumiwa katika uwindaji
- Kulungu
- Elk
- Nyati
- Caribou
- Moose
- Ngamia n.k
Madhara ya Ugonjwa wa Brucella(Complications)
Brucellosis inaweza kuathiri karibu sehemu yoyote ya mwili wako, pamoja na mfumo wako wa uzazi, ini, moyo na mfumo mkuu wa neva. Brucellosis sugu inaweza kusababisha shida katika kiungo kimoja tu au katika mwili wako wote. Shida zinazowezekana ni pamoja na:
• Kuvimba kwa safu ya ndani ya vyumba vya moyo (endocarditis).
Hii ni mojawapo ya matatizo makubwa zaidi yanayotokana na brucellosis. Endocarditis isiyotibiwa inaweza kuharibu vali za moyo na ndio sababu kuu ya vifo vinavyohusiana na brucellosis.
• Ugonjwa wa Arthritis.
Hali hii huhusisha Kuvimba kwa viungo kunakoambatana na maumivu, ugumu na uvimbe kwenye viungo, haswa magoti, nyonga, vifundo vya miguu, mikono na mgongo,
• Pia Kuvimba kwa viungo kwenye mgongo wako (spondylitis) au viungo vinavyounganisha mgongo wa chini na pelvis (sacroiliitis), Hali hii inaweza kuwa ngumu sana kutibu na inaweza kusababisha uharibifu wa kudumu.
• Kuvimba na maambukizi ya korodani (epididymo-orchitis).
Bakteria wanaosababisha brucellosis wanaweza kuambukiza epididymis, mirija iliyojikunja inayounganisha vas deferens na korodani. Kutoka hapo, maambukizi yanaweza kuenea kwenye korodani yenyewe, na kusababisha uvimbe na maumivu, ambapo hali hii inaweza kuwa kali.
• Kuvimba na maambukizi ya wengu na ini.
Brucellosis inaweza pia kuathiri wengu na Ini, Kisha kufanya Viungo hivi kukua zaidi ya ukubwa wake wa kawaida.
• Maambukizi ya mfumo mkuu wa neva.
Haya ni pamoja na magonjwa yanayoweza kutishia maisha kama vile kuvimba kwa utando unaozunguka ubongo na uti wa mgongo (meninjitisi) au kuvimba kwa ubongo wenyewe (encephalitis). Haya yote huweza kuwa madhara ya Ugonjwa wa brucella.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!