Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA MFUMO WA UMEME WA MOYO(chanzo chake)



MOYO

• • • • •

UGONJWA WA MFUMO WA UMEME WA MOYO(chanzo chake)


Kutokana na maelezo ya Dr. Peter Kisenge Machi 2020, Dactari bingwa wa moyo katika Taasisi ya moyo ya jakaya Kikwete alielezea kwamba;


Ugonjwa wa mfumo wa umeme wa moyo huhusisha hali ya kuvurugika kwa mfumo mzima wa umeme ndani ya moyo kitu ambacho hupelekea mapigo ya moyo kuwa juu sana au kuwa chini sana hali ambayo sio sawa katika mwili wa binadamu.


Kazi kubwa ya umeme huo ndani ya moyo nikusaidia moyo katika shughuli zake za kusukuma damu kwenda katika maeneo tofauti tofauti ya mwili wa binadamu.


Namnukuu maneno yake;


“Mapigo ya moyo yanakuwa chini ya 40 kwa dakika. Mgonjwa anapata shida anapokuwa anafanya shughuli zake anachoka au wakati mwingine anaanguka na anapata shida sana,” amesema Dk Kisenge.


•Soma: Madhara ya Kubana Mkojo kwa Muda mrefu


CHANZO CHA UGONJWA HUU WA MFUMO WA UMEME NDANI YA MOYO NI PAMOJA NA;


- Mgonjwa kuwa na tatizo la mishipa ya damu


- Mgonjwa kuwa na umri mkubwa mfano miaka; 55,70 N.K


- Hali ya kimaumbile ya mtu


- Pia watu wenye magonjwa ya kurithi wapo kwenye hatari ya kupatwa na ugonjwa huu wa umeme ndani ya moyo

N.K


Cc; @Mwananchi (source.)


FAHAMU HII KUHUSU MOYO


Tofauti na viungo vingine vya mwili, moyo umeumbwa na msuli maalum ambao hufanya kazi toka ukiwa tumboni mpaka siku unafariki bila kusimama hata sekunde moja.


Msuli huo hupiga mara 70 mpaka 100 ndani ya dakika moja, mara 100,000 kwa siku  na mara 40,000,00 kwa mwaka.


Kila moyo unapopiga husukuma damu Sawa na ujazo wa kikombe;


Damu hii husukumwa kwa nguvu inayoiwezesha kuzunguka bila kusimama ndani ya mtandao wa mishipa yenye urefu sawa na kilomita 100,000 kufikia seli zote za mwili na kuzipa oksijeni na virutubisho


Ikitokea damu haijafikia seli hai ya mwili basi hiyo seli huanza kufariki ndani ya muda mfupi wastani kuanzia dakika kuendelea.


(📝NormanJonasMD)


•Soma: Madhara ya Kubana Mkojo kwa Muda mrefu



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LINALOKUSUMBUA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments