MOYO
• • • • •
UGONJWA WA SHAMBULIO LA MOYO AU HEART ATTACK(chanzo,dalili,tiba)
Huu ni ugonjwa ambao hutokea kwenye moyo, na ugonjwa huu huweza kumpata mtu yoyote,mwanamke,mwanaume, kijana au Mzee.
CHANZO CHA UGONJWA WA SHAMBULIO LA MOYO AU HEART ATTACK
Ugonjwa wa shambulio la moyo hutokana na kuwa na shida kwenye mishipa ya damu ndani ya moyo,ambapo mishipa hiyo huziba kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo sababu ya mafuta kuzidi mwilini.
DALILI ZA UGONJWA WA SHAMBULIO LA MOYO AU HEART ATTACK NI PAMOJA NA;
1. Mgonjwa kupata shida sana wakati wa kupumua au wakati wa kuvuta na kutoa hewa
2. Mgonjwa kupatwa uchovu wa mwili uliokithiri
3. Mgonjwa kupatwa na maumivu makali ya kifua ambayo huweza kusambaa katika sehemu mbali mbali za mwili kama vile mabegani na shingoni
4. Mgonjwa kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika mara kwa mara
5. Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa
6. Mapigo ya moyo kwa mgonjwa kubadilika na kwenda kwa kasi sana
7. Mgonjwa kupatwa na hali ya kutoa jasho jingi mwilini
N.K
WATU AMBAO HUWEZA KUPATWA NA UGONJWA WA SHAMBULIO LA MOYO KWA HARAKA ZAIDI NI PAMOJA NA;
- Wavutaji wa sigara
- Wanywaji wa pombe
- Watu wenye magonjwa mengine kama ugonjwa wa presha
- Watu wenye matatizo la Sukari
- Watu wenye uzito mkubwa au wanene sana
MATIBABU YA UGONJWA WA SHAMBULIO LA MOYO AU HEART ATTACK
- Ugonjwa huu huhusisha matibabu ya aina mbali mbali kama vile;
Mgonjwa kuongezewa hewa ya Oxygen kwa kutumia vifaa maalumu kwani tayari atakuwa ana shida ya kukosa hewa ya kutosha mwilini
Mgonjwa kupewa dawa mbali mbali kama za kutuliza maumivu pamoja na Dawa ambazo huweza kuyeyusha mafuta yote kwenye mishipa ya damu kwenye moyo kama vile; clopidogrel
Mgonjwa Kufanyiwa upasuaji kama hatua ya juu ya kimatibabu
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!