VYAKULA VYA KUZINGATIA KWA MGONJWA WA SUKARI (je mgonjwa wa Sukari anatakiwa aleje?)
SUKARI
• • • • • •
VYAKULA VYA KUZINGATIA KWA MGONJWA WA SUKARI (je mgonjwa wa Sukari anatakiwa aleje?)
Moja ya vitu muhimu sana vya kuzingatia kwa Mgonjwa wa sukari ni pamoja na lishe,aina za vyakula anavyokula na jinsi ya kula vyakula hivo. Na kadri unavyojua kudhibiti ulaji wako ndivo unavyopata urahisi wa kudhibiti sukari yako mwilini.
Kuna dhana mbali mbali za watu mtaani kwamba ukishaumwa ugonjwa wa sukari basi wewe kwa asilimia kubwa kila aina ya chakula kwako kula ni vigumu, na huku wengine wakijenga dhana kwamba labla wewe ni mtu maalumu sana ambaye unatakiwa kupewa vyakula maalum kabsa.
Kwa kifupi tu ni kwamba,Mgonjwa wa sukari hana umaalumu huo ambao watu huwatishia sana watu hawa, ila kwa ufupi tu ni kwamba,Mgonjwa wa sukari ana weza kula kila aina ya chakula ukiacha tu vyakula vya sukari.
ANGALIZO; Vyakula ambazo ni jamii ya wanga Mfano Wali, huwa baada ya mchakato wa kuvunja vunja chakula mwisho tunapata sukari, Hivo hata kama vyakula hivi havina sukari ila ukila kwa kiwango kikubwa basi hata sukari yako mwilini itaongezeka na kuanza kukuletea madhara mbali mbali kwa wewe ambaye una ugonjwa wa kisukari.
Hivo basi unaweza kuendelea kula vyakula vya wanga kama Ugali,Wali N.K kwa kiasi kidogo huku ukila Mboga za majani kwa wingi sana.
Kwahyo,Mpangalio wa ulaji wa chakula kwa mtu mwenye sukari ni kuhakikisha anakula vyakula vyote ambavyo haviwezi kuongeza sukari mwilini kwani tayari ana sukari ya kutosha mwilini. Epuka unywaji wa soda nyingi kwani soda pia huongeza kiwango cha sukari mwilini, Na pia epuka kuweka sukari nyingi kwenye chai N.K
Ni vizuri kuendelea kupima na kuchunguza kiwango cha sukari yako mwilini mara kwa mara na pia kujua dalili zote endapo pakitokea mabadiliko ya sukari yasio yakawaida ili upate msaada na tiba kwa haraka.
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!