Connect with us

afyaclass tips

DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA(chanzo,dalili na tiba)

Published

on

  MALARIA

• • • • •

DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA(chanzo,dalili na tiba)


CHANZO CHA UGONJWA WA MALARIA


Ugonjwa wa Malaria ni ugonjwa ambao husababishwa va vimelea vya magonjwa viitwavyo Plasmodium.


Vimelea hivi vipo vya aina mbali mbali kama vile; Plasmodium vivax,plasmodium malariae,plasmodium falciparum, plasmodium ovale 


•Soma: Ugonjwa wa Tezi Dume, chanzo,Dalili zake pamoja na Matibabu yake


DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA NI PAMOJA NA;


1. Joto la mwili la mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa


2. Mgonjwa kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika


3. Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa


4. Mgonjwa kuhisi hali ya kizunguzungu kikali


5. Hamu ya kula au appetite ya chakula kupotea


6. Wakati mwingine mgonjwa kutoa jasho sana


7. Mgonjwa kuwa na dalili zote za kuchanganyikiwa au kuweweseka sana wakati malaria ikiwa kali


VIPIMO;


Moja ya vipimo ambavyo hutumika kupima ugonjwa wa Malaria ni pamoja na kipimo cha Damu kwa kutumia kifaa kinachoitwa MRDT.


MATIBABU YA UGONJWA WA MALARIA


Mgonjwa wa malaria hutibiwa baada ya kufanyiwa vipimo kwa kutumia dawa mbali mbali kama vile; ALU au mseto, Malaffin, Quinine N.K


•Soma: Ugonjwa wa Tezi Dume, chanzo,Dalili zake pamoja na Matibabu yake


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

afyaclass tips

KUPATA MAARIFA KUHUSU AFYA YAKO(huduma)

Published

on

 AFYA TIPS

• • • • •

KUPATA MAARIFA KUHUSU AFYA YAKO(huduma)


Katika ulimwengu wa sasa ni dhahiri kwamba dunia ipo kiganjani kwako, Hivo basi kwa kutumia tu simu yako ya mkononi unaweza kupata faida nyingi sana, ikiwa ni pamoja na faida ya kuimarisha afya yako kupitia usomaji wa makala mbali mbali za afya.


Hivo basi, endapo utafahamu jinsi ya kutafta taarifa sahihi mtandaoni, itakusaidia wewe kujifunza vitu vingi ikiwa ni pamoja na kujua dalili za magonjwa mbali mbali ambayo huweza kukupata kwa muda wowote.


Jifunze zaidi mambo yanayohusu afya yako mtandaoni ili kuongeza maarifa zaidi, na kuweza kujikinga na magonjwa mbali mbali hatarishi.


• Soma: Dalili za Ugonjwa wa Fangasi wa kichwani


Unaweza kujifunza kuhusu magonjwa mengi tu ambayo husumbua sana watu kwa hivi sasa na jinsi ya kujikinga na magonjwa hayo, Magonjwa hayo ni kama vile;


1. Ugonjwa wa kansa au Saratani ambapo kuna aina nyingi sana za saratani mfano;


– Kuna saratani ya damu


– Saratani ya matiti


– Saratani ya shingo ya kizazi


– Saratani ya ngozi


– Saratani ya koo


– Saratani ya tezi dume


– Saratani ya mifupa

N.K


2. Ugonjwa wa presha au shinikizo la damu


3. Ugonjwa wa kisukari


4. Magonjwa mbali mbali ya moyo ikiwa ni pamoja na moyo kuwa mkubwa,tatizo la mfumo wa umeme ndani ya moyo  pamoja na mishipa ya damu kuziba ndani ya moyo


5. Uvimbe wa kizazi  pamoja na kuziba kwa mirija ya uzazi kwa wanawake


6. Ugonjwa wa UTI


7. Ugonjwa wa Fangazi za aina mbali mbali kama vile;


– Fangasi wa sehemu za siri


– Fangasi wa kwenye damu


– Fangasi wa miguuni


– Fangasi wa ulimi


– Fangasi wa mdomoni

N.K


8. Ugonjwa wa vidonda vya tumbo


9. Maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanamke yaani PID


10. Tatizo la mvurugiko wa vichocheo mwilini yaani hormone imbalance


11. Magonjwa mbali mbali ya zinaa kama vile; kisonono, Chlamydia kaswende pamoja na ugonjwa wa Ukimwi


12. Pamoja na magonjwa mengine ambayo sikuyataja hapa


Soma: Dalili za Ugonjwa wa Fangasi wa kichwani


Hivo ongeza maarifa zaidi kupitia simu yako ya mkononi, na fwatilia makala mbali mbali za afya ili upate faida zaidi kwenye huu ulimwengu wa sayansi na Teknologia


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Continue Reading

afyaclass tips

UGONJWA WA WENGU(chanzo,dalili na tiba)

Published

on

 WENGU

• • • • • •

UGONJWA WA WENGU(chanzo,dalili na tiba)

Ugonjwa wa wengu au bandama na kwa kitaalam hujulikana kama Spleen, kwanza fahamu kwamba, wengu ni kiungo muhimu sana kwenye mwili wa binadamu ambapo kinahusika katika utendaji wa kazi mbali mbali mwilini ikiwa ni pamoja na kusaidia mmeng’enyo wa chakula, kusafisha damu N.K

Endapo kiungo hiki cha wengu kimeshambuliwa na magonjwa, basi mtu huanza kuonyesha dalili mbali mbali kwenye mwili wake.

• Soma: Ugonjwa wa Mfumo wa Umeme Ndani ya Moyo,chanzo,dalili na Tiba yake

DALILI ZA UGONJWA WA WENGU NI PAMOJA NA;

• Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa

• Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya kula chakula

• Mgonjwa kupata maumivu makali sehemu ya wengu hasa kama wengu au bandama imevimba

• Mgonjwa kuhisi uzito usio wa kawaida upande wa kushoto karibu na kitovu

• Uzito wa mwili kuporomoka kwa kiasi kikubwa au mgonjwa kukonda

• Mgonjwa kupatwa na kichefu chefu pamoja na kutapika

• Mgonjwa kupata matatizo mbali mbali katika kujisaidia

N.K

• Soma: Ugonjwa wa Mfumo wa Umeme Ndani ya Moyo,chanzo,dalili na Tiba yake

MATIBABU YA UGONJWA WA WENGU

– Zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kutibu magonjwa ya wengu ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa mbali mbali jamii ya Antibiotics,Antihistamines N.K

Pamoja na njia ya kufanyiwa upasuaji kama njia nyingine ya kimatibabu kwa mtu mwenye Ugonjwa wa wengu.

• Soma: Ugonjwa wa Mfumo wa Umeme Ndani ya Moyo,chanzo,dalili na Tiba yake

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2017 Zox News Theme. Theme by MVP Themes, powered by WordPress.