DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA(chanzo,dalili na tiba)

  MALARIA

• • • • •

DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA(chanzo,dalili na tiba)


CHANZO CHA UGONJWA WA MALARIA


Ugonjwa wa Malaria ni ugonjwa ambao husababishwa va vimelea vya magonjwa viitwavyo Plasmodium.


Vimelea hivi vipo vya aina mbali mbali kama vile; Plasmodium vivax,plasmodium malariae,plasmodium falciparum, plasmodium ovale 


•Soma: Ugonjwa wa Tezi Dume, chanzo,Dalili zake pamoja na Matibabu yake


DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA NI PAMOJA NA;


1. Joto la mwili la mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa


2. Mgonjwa kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika


3. Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa


4. Mgonjwa kuhisi hali ya kizunguzungu kikali


5. Hamu ya kula au appetite ya chakula kupotea


6. Wakati mwingine mgonjwa kutoa jasho sana


7. Mgonjwa kuwa na dalili zote za kuchanganyikiwa au kuweweseka sana wakati malaria ikiwa kali


VIPIMO;


Moja ya vipimo ambavyo hutumika kupima ugonjwa wa Malaria ni pamoja na kipimo cha Damu kwa kutumia kifaa kinachoitwa MRDT.


MATIBABU YA UGONJWA WA MALARIA


Mgonjwa wa malaria hutibiwa baada ya kufanyiwa vipimo kwa kutumia dawa mbali mbali kama vile; ALU au mseto, Malaffin, Quinine N.K


•Soma: Ugonjwa wa Tezi Dume, chanzo,Dalili zake pamoja na Matibabu yake


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!