HPV
• • • • •
FAHAMU KUHUSU KIRUSI CHA HUMAN PAPILLOMA VIRUS(HPV)
Human papilloma virus au kwa kifupi HPV ni kirusi ambacho husambaa kwa asilimia kubwa kwa Njia ya kufanya tendo la ndoa au kujamiiana,
Hivo watu ambao wanafanya mapenzi bila kinga, Wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile, au aina yoyote ya sex( Vaginal sex,anal sex,oral sex) wote wapo kwenye hatari ya kupata kirusi hiki.
MAGONJWA AMBAYO HUSABABISHWA NA KIRUSI HIKI CHA HPV
- HPV au Human papilloma virus huweza kusababisha aina mbali mbali za kansa kwenye mwili wa binadamu kama vile;
1. Kansa ya shingo ya kizazi au kwa kitaalam hujulikana kama Cervical cancer
2. Kansa ya njia ya haja kubwa
3. Kansa ya uume kwa wanaume
4. Kansa ya ukeni kwa wanawake
5. Kansa ya kooni (throat cancer)
N.K
- Asilimia kubwa ya watu wenye maambukizi ya HPV hupata vipele au genital warts kwa wanawake, maumivu wakati wa mapenzi, kuwashwa, kutoa damu wakati wa mapenzi n.k
WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA HPV
- Watu ambao wanafanya mapenzi bila kinga
- Watu wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile
- Watu wenye shida ya kinga ndogo ya mwili mfano wale wenye magonjwa kama vile; UKIMWI
- Watu wenye umri mkubwa zaidi
N.k
MATIBABU YA MAAMBUKIZI YA HPV
- Maambukizi ya human papilloma virus(HPV) hupona yenyewe hasa kwa watoto wadogo, lakini kwa watu wazima ni ngumu kidogo, na kwa bahati mbaya hakuna dawa ya moja kwa moja ya kudhibiti kirusi hiki,
bali matibabu yapo kwa ajili ya kudhibiti dalili zinazoletwa na kirusi hiki kama ilivyo matibabu ya magonjwa mengi ambayo huletwa na Virusi mbali mbali.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA MAGONJWA MBALI MBALI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!