FAHAMU KUHUSU VIRUSI VYA CORONA NA UGONJWA WA COVID 19(chanzo,dalili,madhara,tiba)
COVID 19
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU VIRUSI VYA CORONA NA UGONJWA WA COVID 19(chanzo,dalili,madhara,tiba)
CORONA; Ni Virusi ambavyo kwa kiasi kikubwa hushambulia Mfumo mzima wa Upumuaji au hewa kwa ujumla wake na virusi hawa huweza kushambulia binadamu na wanyama pia.
COVID-19; Huu ni ugonjwa ambao husababishwa na virusi wanaojulikana kwa Jina la Corona. Hivo basi, chanzo cha Ugonjwa wa COVID 19 ni maambukizi na mashambulizi ya Virusi wanaojulikana kwa jina la Corona.
Chimbuko la Jina COVID 19, Linatokana na kugundulika kwa Virusi vya Corona nchini CHINA mwezi DECEMBER mwaka 2019, hapo ndyo jina la COVID 19 Likatokea(ikiwa na maana ya ugonjwa wenyewe pamoja na mwaka ulipogundulika)
DALILI ZA UGONJWA WA COVID 19 NI PAMOJA NA;
✓ Mgonjwa kupatwa na kikohozi kikavu
✓ Joto la mwili kwa Mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa kali
✓ Mgonjwa kupatwa na mafua ambayo hutoka mara kwa mara kama maji
✓ Mgonjwa kupata shida sana ya upumuaji
✓ Mgonjwa kubanwa mbavu wakati wa kupumua
✓ Mgonjwa kupata maumivu ya kifua
✓ Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa
✓ Mgonjwa kukosa pumzi
✓ Mwili kuchoka sana
N.K
WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATWA NA UGONJWA HUU
- Watu ambao hukaa sana maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu au sehemu ambapo kuna mkusanyiko mkubwa wa watu kama vile sokoni,stend, kwenye sherehe,mikutano, au kwenye misiba.
- Watu ambao wana magonjwa ya muda mrefu kama vile, magonjwa ya Figo, Ugonjwa wa Sukari,shinikizo la damu au Presha
- Watu ambao wana magonjwa ambayo husababisha upungufu wa kinga mwilini kama vile ukimwi N.K
- Watu ambao wana magonjwa mengine ya mfumo wa hewa au upumuaji,matatizo ya mapafu N.K
- watumishi wa afya ambao huhudumia wagonjwa wa COVID 19
- Watu ambao tayari wana mgonjwa wa COVID 19 kwenye Familia yao
MATIBABU YA UGONJWA HUU
- Mpaka sasa hakuna tiba ya moja kwa moja ya kutibu na kumaliza tatizo hili,ila kuna dawa za kudhibiti dalili mbali mbali zinazosababishwa na ugonwa huu.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA MAGONJWA MENGINE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!