KAZI YA HORMONE YA KIUME TESTOSTERONE,ATHARI ZA UPUNGUFU WAKE(pamoja na dalili)

HORMONE YA KIUME

• • • • • •

KAZI YA HORMONE YA KIUME TESTOSTERONE,ATHARI ZA UPUNGUFU WAKE(pamoja na dalili)

Testosterone ni homoni ya kiume ambayo hufanya kazi nyingi sana mwilini.

KAZI ZA HORMONE HII YA KIUME AU TESTOSTERONE MWILINI NI PAMOJA NA;

- Kusababisha mabadiliko ambayo mwanaume huyapata kipindi cha ukuaji wake au kipindi cha balehe; kama vile;

• Mwanaume kupanuka kifua na kuwa na umbo la kiutu uzima

• Mwanaume kuwa na sauti nzito

• Maumbile ya mwanaume kuongezeka ukubwa au via vya uzazi vya mwanaume kukomaa

• Mwanaume kuota ndevu

• Mwanaume kuota nywele kifuani,na sehemu mbali mbali za mwili kama vile; Kwapani,Sehemu za siri N.K

• Mwanaume kuanza kuwa na hamu sana ya kufanya mapenzi

• Mwanaume kuanza kuzalisha na kumwaga shawaha au mbegu za kiume

N.K

 SABABU ZA UPUNGUFU WA HORMONE HII YA KIUME NI PAMOJA NA;

1. Maambukizi  ya magonjwa mbali mbali ya zinaa

2. Kuwa na tatizo la maambukizi katika mfumo wa mkojo ya muda mrefu au Uti Sugu

3. Mwanaume Kuumia kwenye korodani kutokana na sababu mbali mbali kama vile; kupigwa ngumi,ajali, kugongwa kwa nguvu na mpira au namna yoyote ile, kuendesha baskeli kwa muda mrefu, hii husababisha msuguano wa korodani

4. Tatizo la korodani kutokushuka chini siku au wakati mtoto anazaliwa, Hii huweza kusababisha upungufu wa hormone hii ya kiume pamoja na upungufu wa mbegu za kiume

5. Matumizi ya pombe kupita kiasi

6. Kuwa na shida ya Uzito mkubwa 

7. Mwanaume kuwa na Kiribatumbo

8. Mwanaume Kutokufanya mazoezi

(Unashauriwa kufanya mazoezi angalau kwa dakika 25-30 kila siku)

9. Mwanaume kuwa na maradhi ya moyo kama vile moyo kufeli N.K

10. Au Mwanaume kuwa na maradhi yoyote yanayozuia hewa isifike vizuri mwilini

11. Mwanaume kuwa na Matatizo ya ini

12. mwanaume kuwa na Tatizo la Figo

13. Mwanaume kuwa na maambukizi ya Ukimwi au HIV

14. Pia tatizo hili huweza kuwa la Kurithi katika familia au koo flani

DALILI ZA UPUNGUFU WA HORMONE HII YA KIUME NI PAMOJA NA;

1. Mwanaume kukosa kabsa hamu ya tendo la ndoa

2. Mwanaume Kutokufurahia kabsa tendo la ndoa wakati anashiriki

3. Mwanaume kutosimamisha vizuri uume wake au kuwa na shida ya upungufu wa nguvu za kiume

4. Matiti kuwa makubwa kama mwanamke

5. Sauti kuanza kuwa nyembamba kama mwanamke

6. Mwanaume kuanza kuwa na umbo la kike

7. Mwanaume Kupoteza ndevu zake

8. Nywele maeneo ya tumboni, kifuani NK huanza kupotea

9. Kuwa na shida ya mifupa kuuma

10. Mwili kuwa mchovu sana  kutokana na kuathiriwa kwa chembechembe za damu ambazo husafirisha hewa ya oxygen mwilini

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!