UZAZI
• • • • • •
MAISHA BAADA YA KUTUMIA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO
Inategemea uliamua kutumia njia gani ilipofikia hatua ya kuamua kupanga uzazi. Je ni njia ya muda mfupi, Njia ya muda mrefu, njia ya kudumu, Njia ya kisasa au Njia ya Asili.
Na kila aina ya njia huweza kusababisha mabadiliko katika nama,mtindo au Staili ya maisha yako katika Familia.
- Kuna baadhi ya Njia huweza kukusababishia mabadiliko ya siku zako za hedhi tofauti na mwanzoni ulivyozoea kuishi
- Kuna baadhi ya njia huweza kukusababishia ukablid kwa muda mrefu na damu nyingi tofauti ba ulivyozoea kuishi
- Kuna Baadhi ya njia huweza kukufanya uwe mtu wa kuumwa na kichwa sana mara kwa mara
- Kuna baadhi ya njia huweza kukusababishia uwe mtu wa kutembea na dawa kila mahali
- Kuna baadhi ya njia huweza kukuletea kizunguzungu kikali
- Kuna baadhi ya njia huweza kubadilisha hata kula yako
- Kuna baadhi ya njia huweza kukufanya uwe mnene sana au uwe mwembamba sana
- Kuna baadhi ya njia huweza kukufanya uwe mtu wa kutapika tapika na kichefuchefu mara kwa mara
- Kuna baadhi ya njia huweza kukufanya usifurahie sana tendo la ndoa
N.K
ushauri wangu kwako, Katika kupanga uzazi, nilazima ukutane na wataalam wa afya muongee kwa kina,wakuonyeshe na kukuelezea kila aina ya Njia ya kupanga uzazi pamoja na faida na hasara zake, Na mshauriane njia gani ni salama kwako kulingana na mwili wako na Afya yako.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!