Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA NGOZI KUKAKAMAA NA KUWA KAVU SANA



 NGOZI

• • • • •

TATIZO LA NGOZI KUKAKAMAA NA KUWA KAVU SANA


Tatizo la ngozi kukakamaa au kuwa kavu sana huweza kuwa hali ya kawaida ambayo huchangiwa na sababu mbali mbali za kawaida kama vile; Hali ya baridi sana, hali ya joto sana,matumizi ya baadhi ya sabuni za kuogea, ngozi kukosa mafuta ya kupaka n.k


Japo pia hili huweza kuwa ni tatizo kabsa ambalo huweza kusababishwa na baadhi ya magonjwa.


Magonjwa ya ngozi au maambukizi mbali mbali ya vimelea vya magonjwa kama vile bacteria,virusi au Fangasi (ambapo hapa ni tatizo) huweza kusababisha hali hii.


TATIZO LA NGOZI KUKAKAMAA NA KUWA KAVU SANA


Hali hii huweza kuwa ni tatizo ambalo linahitaji msaada wa kimatibabu kama shida hii huambatana na vitu vifuatavyo;


1. Kukamaa kwa ngozi, ngozi kukauka ambayo huambatana na na miwasho mikali kwenye ngozi


2. Ngozi kukakamaa lakini ikiambatana na kuwepo kwa vidonda kwenye ngozi


3. Hali ya ngozi kukakamaa ambayo huambatana na michubuko ya ngozi


4. Hali ya ngozi kukakamaa au kuwa kavu ikiambatana na kubadilika rangi na kuwa nyekundu


5. Hali ya ngozi kukakamaa na kuchanika yenyewe


6. Hali ya ngozi kuwa kavu ambayo huambatana na maumivu makali

n.k


Endapo unapata dalili kama hizi kutana na wataalam wa afya kwa Ajili ya msaada wa kimatibabu.


Pia zingatia vitu hivi;


- Epuka matumizi ya sabuni za kuogea zenye kemikali sumu


- Epuka kukaa kwenye jua kwa muda mrefu


- Usiache kupaka mafuta kwenye ngozi yako hasa kipindi cha baridi kali


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.








Post a Comment

0 Comments