UGONJWA WA ANEMIA(tatizo la upungufu wa damu mwilini)

   ANEMIA

• • • •

UGONJWA WA ANEMIA(tatizo la upungufu wa damu mwilini)


Kama nilivyokwisha kueleza hapo juu kwenye kichwa cha makala hii, Ugonjwa wa anemia ni ugonjwa wa upungufu wa damu mwilini, ambapo upungufu  huu hutokana na upungufu wa seli nyekundu za damu yaani Red blood cells pamoja na upungufu wa chembe chembe nyekundu za damu yaani haemoglobin.


Ambapo upungufu huo huchangiwa na sababu mbali mbali kama ifuatavyo;


SABABU ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI(ANEMIA)


- Tatizo la ukosefu wa madini ya chuma ambayo ndyo hutumika kutengeneza chembe chembe nyekundu za damu yaani haemoglobin


- Upungufu wa damu mwilini ambao huchangiwa na kiwango kikubwa cha damu kupotea mwilini kutokana na sababu mbali mbali kama vile; kupata ajali, mama mjamzito wakati wa kujifungua kumwaga damu nyingi N.K


- Kuwa na tatizo la sickle cell ambalo husababisha seli nyekundu za damu kuwa na umbo au shape isiyoyakawaida hivo kufa mapema kabla ya kukomaa, hali ambayo hupelekea kuwe na tatizo la upungufu wa seli nyekundu za damu pamoja na upungufu wa damu mwilini


- Kushambuliwa na magonjwa mbali mbali kama Malaria, pamoja na minyoo jamii ya hookworms.


- Tatizo la mifupa ya mwili kushindwa kutengeneza seli nyekundu za damu kutokana na athari ya vitu mbali mbali kama vile; matumizi ya baadhi ya Dawa au baadhi ya makemiko


DALILI ZA UGONJWA WA ANEMIA NI PAMOJA NA


- ngozi ya mwili kubadilika na kukakamaa


- Kubadilika rangi ya macho na kuwa nyeupe


- Kubadilika rangi ya lips za mdomo kuwa nyeupe


- Kubadilika rangi ya viganja vya mikono na kuwa nyeupe


- Kuwa na hali ya kizunguzungu na kupepesuka


- Mwili kuchoka sana na kukosa nguvu kabsa


- Kuwa shida ya mapigo ya moyo kwenda kwa kasi zaidi


- Kuwa na tatizo la kushindwa kupumua



MATIBABU YA UGONJWA WA ANEMIA


- Matibabu ya tatizo la upungufu wa damu mwilini au anemia hutegemea na chanzo chake, japo kwa ujumla wake matibabu ya tatizo hili ni pamoja na;


- Kuongezewa damu kwa watu wenye uhitaji wa kuongezewa damu


- Ulaji wa vidonge vya kuongeza damu maarufu kama FEFOL au vidonge vya folic acid


- Kula mboga za majani kwa wingi hasa matembele


- Kula vyakula vyenye vitamin B12 kwa wingi pamoja na madini ya Chuma


- Kupewa dawa za kutibu malaria kama vile Mseto(ALU) pamoja na dawa zingine za malaria


- Kupewa dawa za kutibu minyoo kama vile Albendazole,mebendazole N.K



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584






0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!