HOMA YA MAPAFU
• • • • • •
UGONJWA WA HOMA YA MAPAFU AU PNEUMONIA(chanzo,dalili,tiba)
Ugonjwa wa homa ya mapafu au pneumonia ni ugonjwa ambao huhusisha kuvimba kwa vifuko vya hewa ndani ya mapafu,ambapo inaweza kuwa pafu moja au mapafu yote mawili.
Ambapo shida hii huweza kusababishwa na vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria(mfano;Streptococcus pneumoniae) ,Fangasi au Virusi.
Maambukizi haya husababisha kuvimba kwa vifuko vya hewa ndani ya mapafu kutokana na kujaa kwa maji au usaha ndani ya vifuko hivi vya hewa na kuleta madhara mbali mbali kama vile; Mgonjwa kukohoa sana, homa, kupata shida ya upumuaji N.K
DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA MAPAFU NI PAMOJA NA;
- Mgonjwa kupata shida sana wakati wa kupumua
- Mgonjwa kukohoa sana mara kwa mara
- Joto la mwili la mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa
- Mgonjwa kupata maumivu makali ya kifua wakati wa kuvuta na kutoa hewa
- Mgonjwa kutoa jasho sana mwilini
- Mgonjwa kuchoka kupita kiasi
- Mgonjwa kupatwa na hali ya kutetemeka mwili
- Mgonjwa kusikia kichefuchefu na kutapika
- Wakati mwingine mgonjwa kuharisha
N.K
WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA HOMA YA MAPAFU
- Watoto wenye umri chini ya miaka miwili
- Watu wazima mfano miaka 70
- Walevi wa pombe
- Wavutaji wa Sigara
- Wenye magonjwa ambayo hushusha kinga ya mwili kama vile UKIMWI
- Watu wenye magonjwa mbali mbali ya Moyo
- Watu wenye magonjwa mengine ya mapafu
- Watu wenye ugonjwa wa kisukari N.K
MATIBABU YA UGONJWA WA HOMA YA MAPAFU
- Matibabu ya ugonjwa huu wa homa ya mapafu huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali jamii ya Antibiotics N.K
Lakini pia kuna chanjo ambazo mtu huweza kupata ili kuzuia mtu asipatwe na ugonjwa huu wa homa ya mapafu.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!