CARDIAC ARREST
• • • • •
UGONJWA WA MOYO WA CARDIAC ARREST(chanzo,dalili na tiba yake)
Cardiac arrest, Huu ni ugonjwa ambapo moyo wa mtu husimama kufanya kazi kwa gafla hali ambayo hupelekea mtu kukosa hewa, kupoteza fahamu na hata kupoteza maisha kabsa.
CHANZO CHA TATIZO LA CARDIAC ARREST
Chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni hitilifu ambayo hutokea kwenye mfumo wa umeme ndani ya moyo, hali ambayo hupelekea moyo kushindwa kufanya kazi zake ikiwemo kazi ya kusuka damu kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wako
DALILI ZA UGONJWA HUU WA CARDIAC ARREST
- Mtu kushindwa kupumua kabsa na kukosa hewa yakutosha mwilini
- Mtu kupoteza fahamu
- Mtu kudondoka gafla
- Kupata uchovu wa mwili usio wakawaida
- Ngozi ya mwili kuanza kukakamaa na kusinyaaa kwa baadhi ya wagonjwa
- Mapigo ya moyo kubadilika kabsa na moyo kupiga kwa kasi sana kuliko kawaida
- Maumivu makali ya kifua
- Mapigo ya moyo kushuka au kuwa chini sana au kutokusikika kabsa
- Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa
- Mgonjwa kupatwa na kizunguzungu kikali
WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;
1. Wavutaji wa sigara
2. Watu ambao hutokea kwenye familia zenye historia ya kuumwa magonjwa ya moyo
3. Watu ambao ni wanene au wenye uzito kupita kiasi
4. Watu wenye matatizo ya shinikizo la damu au Presha
5. Watu wenye kiwango kikubwa cha Cholesterol mwilini
6. Watu wenye ugonjwa wa Kisukari
7. Wanywaji wa pombe
N.K
MATIBABU YA UGONJWA WA CARDIAC ARRREST
- Tatizo hili huhitaji msaada wa haraka sana kwani mtu huweza kupoteza maisha haraka zaidi, hivo njia mbali mbali huweza kutumika hospitalin kumsaidia mgonjwa mwene shdia hii kama vile Njia ya; CPR pamoja na DEFIBRILLATION.
- Hivo basi kama mtu ana dalili hivi,akimbizwe hospital mara moja kwa ajili ya msaada wa kimatibabu
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!