WENGU
• • • • • •
UGONJWA WA WENGU(chanzo,dalili na tiba)
Ugonjwa wa wengu au bandama na kwa kitaalam hujulikana kama Spleen, kwanza fahamu kwamba, wengu ni kiungo muhimu sana kwenye mwili wa binadamu ambapo kinahusika katika utendaji wa kazi mbali mbali mwilini ikiwa ni pamoja na kusaidia mmeng'enyo wa chakula, kusafisha damu N.K
Endapo kiungo hiki cha wengu kimeshambuliwa na magonjwa, basi mtu huanza kuonyesha dalili mbali mbali kwenye mwili wake.
• Soma: Ugonjwa wa Mfumo wa Umeme Ndani ya Moyo,chanzo,dalili na Tiba yake
DALILI ZA UGONJWA WA WENGU NI PAMOJA NA;
• Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa
• Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya kula chakula
• Mgonjwa kupata maumivu makali sehemu ya wengu hasa kama wengu au bandama imevimba
• Mgonjwa kuhisi uzito usio wa kawaida upande wa kushoto karibu na kitovu
• Uzito wa mwili kuporomoka kwa kiasi kikubwa au mgonjwa kukonda
• Mgonjwa kupatwa na kichefu chefu pamoja na kutapika
• Mgonjwa kupata matatizo mbali mbali katika kujisaidia
N.K
• Soma: Ugonjwa wa Mfumo wa Umeme Ndani ya Moyo,chanzo,dalili na Tiba yake
MATIBABU YA UGONJWA WA WENGU
- Zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kutibu magonjwa ya wengu ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa mbali mbali jamii ya Antibiotics,Antihistamines N.K
Pamoja na njia ya kufanyiwa upasuaji kama njia nyingine ya kimatibabu kwa mtu mwenye Ugonjwa wa wengu.
• Soma: Ugonjwa wa Mfumo wa Umeme Ndani ya Moyo,chanzo,dalili na Tiba yake
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!