FAHAMU KUHUSU AINA ZA MAKUNDI YA DAMU(BLOOD GROUPS) PAMOJA NA UCHANGIAJI WA DAMU
BLOOD GROUPS
• • • • •
FAHAMU KUHUSU AINA ZA MAKUNDI YA DAMU(BLOOD GROUPS) KWENYE MWILI WA BINADAMU PAMOJA NA UCHANGIAJI WA DAMU
AINA ZA MAKUNDI YA DAMU(BLOOD GROUPS)
Kuna aina kuu NNE(4) za makundi ya Damu ambayo ni;
1. Blood group A
2. Blood group B
3. Blood group AB
4. Blood group O
Lakini kwa kuongezea,bila shaka utaona kila kundi la damu ambalo mtu kapimwa,Huandikiwa alama mbili POSITIVE au NEGATIVE mfano;
Blood group A+, A-, B+,B-, AB+, AB-, O+, O- Je Hizi positive na Negative ni kitu gani?
Hizi Humaanisha Rhesus factor ambapo Kundi lolote la damu lazima liwe POSITIVE- ikiwa na maana kwamba lina Rhesus Factor au NEGATIVE ikiwa na maana kwamba,halina Rhesus factor.
UCHANGIAJI WA DAMU
- Hapana tuna watu wa aina mbili ambao ni MCHANGIAJI WA DAMU yaani DONOR pamoja na anayechangiwa damu au mpokeaji wa damu yaani RECIPIENT
- Tuanze na Maelezo kuhusu Mchangiaji wa Damu yaani donor
1. MCHANGIAJI WA DAMU(DONOR)
(i) Blood group A
- Mtu mwenye Blood group A+, hutoa damu kwa watu wenye Blood group A+ na AB+.
- Mtu mwenye Blood group A-, hutoa damu kwa watu wenye Blood group A-,A+,AB- na AB+.
(ii) Blood group B
- Mtu mwenye Blood group B+ hutoa damu kwa watu wenye Blood group B+ na AB+.
- Mtu mwenye Blood group B- hutoa damu kwa watu wenye Blood group B-,B+,AB- na AB+.
(iii) Blood group AB
- Mtu mwenye Blood group AB+ hutoa damu kwa watu wenye Blood group AB+ peke yake.
- Mtu mwenye Blood group AB- hutoa damu kwa watu wenye Blood group AB- na AB+.
(iv) Blood group O
- Mtu mwenye Blood group O+ hutoa damu kwa watu wenye Blood group O+,A+,B+ na AB+.
- Na Mtu mwenye Blood group O- huyu ni UNIVERSAL DONOR, yaani hutoa damu kwa watu wenye makundi yote ya damu, A+,A-,B+,B-,AB+,AB-,O+ na O-.
2. MPOKEAJI WA DAMU(RECIPIENT)
(i) Blood group A
- Mtu mwenye Blood group A+, hupokea damu kwa watu wenye Blood group A+,A-,O+ na O-.
- Mtu mwenye Blood group A-, hupokea damu kwa watu wenye Blood group A- na O-.
(ii) Blood group B
-- Mtu mwenye Blood group B+ hupokea damu kwa watu wenye Blood group B+,B-,O+ na O-.
- Mtu mwenye Blood group B- hupokea damu kwa watu wenye Blood group B- na O-.
(iii) Blood group AB
- Mtu mwenye Blood group AB+ hupokea damu kwa watu wote yaani ni UNIVERSAL RECIPIENT ,hivo hupokea damu kutoka kwa makundi yote ya damu yaani Blood group A+,A-,B+,B-, AB+,AB-,O+ na O-
- Mtu mwenye Blood group AB- hupokea damu kwa watu wenye Blood group A-,B-,AB- na O-.
(iv) Blood group O
- Mtu mwenye Blood group O+ hupokea damu kwa watu wenye Blood group O+ na O-
- Na Mtu mwenye Blood group O- hupokea damu kwa watu wenye Blood group O-.
KUFAHAMU ZAIDI kuhusu Madhara ya Baadhi ya makundi ya Damu Soma hapa..!!
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!