FAHAMU KUHUSU DAWA ZA ARVs

 ARV

• • • • •

FAHAMU KUHUSU DAWA ZA ARVs


ARVs ni kifupi cha neno antiretroviral drugs, ikiwa na maana ya dawa kwa ajili ya Virusi vya Ukimwi,


Hivo basi ARV sio dawa moja bali ni kundi au mjumuisho wa dawa zote ambazo hutumika kwa Mgonjwa mwenye virusi vya Ukimwi(VVU) na mfano wa dawa hizo ni kama vile;



- Zidovudine


- Tenofovir


- Abacavir


- Lamivudine


- Didanosine


- Emtricitabine

n.k


Dawa hizi sio za kutibu au kuponyesha kabsa Ukimwi bali hufanya kazi ya kupunguza Virusi vya ukimwi (Viral Load) hali ambayo huupa nafasi Mfumo wa kinga ya mwili kupambana vizuri na ugonjwa huu.


Ili dawa hizi zilete matokeo mazuri unashauriwa kutokuacha kutumia dawa kutokana na maelekezo uliyopewa, kwani ni hatari na unaweza kutengeneza hali ya virusi kutokusikia dawa yaani Drug resistance.



KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!