MTOTO KUZALIWA NA MATITI KAMA BINTI ANAYEKUA(chanzo)

 AFYA KWA MTOTO

• • • • • •

MTOTO  KUZALIWA NA MATITI KAMA BINTI ANAYEKUA(chanzo)


Baadhi ya watu hushangaa sana kwamba mbona baadhi ya watoto ambao ndyo wamezaliwa tu lakini wana matiti kabsa kama binti mkubwa anayekua, je hii ni nini?


JIBU; ndyo ipo na inawezekana


Mtoto mdogo huweza kuzaliwa na matiti kama binti anayekuwa, hali hii hutokea na haina madhara yoyote, katika makala hii tunachambua kuhusu chanzo chake.


CHANZO CHA MTOTO KUZALIWA NA MATITI


- Hali hii hutokea kutokana na mtoto mdogo kuwa katika mazingira ya vichocheo vingi vya mama ake pindi akiwa tumboni,


Ambapo tafiti huonyesha kwamba vichocheo vya Estrogen kutoka kwa mama huchangia kwa wastani wa asilimia 70% watoto kuzaliwa na matiti makubwa.


Na hali hii ya kuwa na matiti makubwa hutokea kwa jinsia yoyote ya mtoto( mwanaume au mwanamke)


KUMBUKA; Kadri umri na muda vinavyosogea ndipo hali hii huisha na kupotea yenyewe, hivo mtoto kurudi katika hali yake ya kawaida.


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!