Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA KUHARISHA KINYESI CHA KIJANI HASA KWA WATOTO



 AFYA

• • • •

TATIZO LA KUHARISHA KINYESI CHA KIJANI HASA KWA WATOTO

Tatizo la kuharisha kinyesi chenye rangi ya kijani huweza kutokea hasa hasa kwa watoto wadogo muda mfupi baada ya kunyonyeshwa,

Je nini maana yake? na chanzo chake ni nini? je ni tatizo la kutisha sana?

CHANZO CHA TATIZO LA KUHARISHA KINYESI CHA KIJANI

- Baada ya chakula kufanyiwa umeng'enyaji uchafu au kinyesi hupita katika mfumo huo wa umeng'enyaji yaani Digestive system, 

Baada ya kinyesi kufika kwenye sehemu ya kwanza kabsa ya utumbo mdogo yaani Small intestine hubadilika rangi na kuwa kijani kutokana na kuchanganyika na nyongo(bile),

Halafu baada ya kinyesi kufika kwenye utumbo mkubwa hubadilika tena Rangi, Ndipo rangi ya dark brown ambayo ndyo rangi ya kawaida ya kinyesi hutokea,

✓ Sasa tatizo la mtu kuharisha au kujisaidia kinyesi cha kijani hutokana na kinyesi hiki baada ya kubadilishwa rangi kuwa kijani ndani ya utumbo mdogo hupita kwa haraka sana kwenye utumbo mkubwa, 

kiasi kwamba mchakato wa kubadilisha rangi ya kinyesi kuwa dark brown haujafanyika,

Hapo ndipo mtu hujisaidia kinyesi chenye rangi ya kijani

KUMBUKA; Hali hii huwatokea sana watoto kwenye hatua za mwanzoni lakini haina madhara yoyote na rangi ya kinyesi itabadika yenyewe bila tiba yoyote

- Pia ulaji mkubwa wa vyakula vyenye rangi ya kijani huweza kuongeza uwezakano wa mtu kujisaidia kinyesi cha rangi ya kijani

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.