TUMBO
• • • • •
TATIZO LA MVURUGIKO WA TUMBO(chanzo,dalili na tiba)
✓ Tatizo la mvurugiko wa tumbo ni tatizo ambalo huhusisha dalili mbali mbali kama vile;
- Tumbo kunguruma sana
- Mtu kupata maumivu ya tumbo
- Mtu kuharisha mara kwa mara
- Mtu kutoa harufu mbaya(kujamba) mara kwa mara
- Na wakati mwingine mtu kupata kichefuchefu pamoja na kutapika
CHANZO CHA TATIZO LA MVURUGIKO WA TUMBO
- Zipo sababu mbalimbali za mtu kupatwa na shida ya mvurugiko wa tumbo, na baadhi ya sababu hizo ni kama vile;
• Kula vyakula ambavyo vinauchafu ndani yake
• Kunywa maji ambayo sio masafi,mfano maji yalichonganyika na vinyesi au uchafu mwingine
• Kula kitu chenye kemikali flani au sumu
• Kula vyakula ambazo vinasababisha gesi kwa kiwango kikubwa
• Kula mchanganyiko wa vyakula vingi, kwa kiasi kikubwa na kwa wakati mmoja
• Mashambulizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria, Minyoo,amiba n.k
MATIBABU YA TATIZO HILI LA MVURUGIKO WA TUMBO
- Tatizo hili huweza kutibiwa kulingana na chanzo cha tatizo, Japo huweza kuhusisha matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; Metronidazole au Flagyl n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!