AFYA YA UZAZI
• • • • •
TATIZO LA MWANAUME KUCHELEWA SANA KUFIKA KILELENI(delayed ejaculation)
Kama ilivyo kwa Wanawake, kuna baadhi ya wanaume pia hukumbwa na tatizo la kuchelewa sana kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa yaani Delayed ejaculation,
je tatizo hili la mwanaume kuchelewa sana kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa husababishwa na kitu gani?
CHANZO CHA TATIZO LA MWANAUME KUCHELEWA SANA KUFIKA KILELENI(delayed ejaculation)
zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia mwanaume kuchelewa sana kufika kileleni wakati akifanya mapenzi na sababu hizo ni kama vile;
- Mwanaume kutumia baadhi ya dawa za hospital na wengine za asili
- Mwanaume kuwa na msongo mkali wa mawazo wakati wa tendo la ndoa
- Mwanaume kukumbwa na hofu pamoja na wasiwasi mkubwa wakati akifanya mapenzi
- Mwanaume kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa wakati huo
- Hali ya kutokuwa na maelewano mazuri ya kimahusiano
- Matatizo mbali mbali ya akili
- Mwanaume kufanyiwa upasuaji sehemu za siri kama vile; Prostate surgery n.k
- Matumizi ya pombe kupita kiasi
- Pia wanaume wanaotumia dawa za presha ya juu,dawa za msongo wa mawazo n.k, huweza kupatwa na tatizo hili
- Tatizo linalohusu kuharibika kwa mfumo wa fahamu au Nerves
- Tatizo la mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini kama vile;
Kuwa na kiwango cha chini sana cha Thyroid hormones yaani Hypothyroidism au kuwa na kiwango cha chini sana cha hormone ya kiume inayojulikana kama Testosterone
- Mwanaume kupatwa na tatizo la mbegu za kiume kwenda kwenye kibofu cha mkojo badala ya kutoka nje hali ambayo hujulikana kama Retrograde ejaculation
- N.K
MATIBABU YATATIZO HILI
- matibabu ya tatizo hili hutegemea sana na chanzo chake, hivo kama una tatizo hili unaweza kuongea na wataalam wa afya kwanza, ili upate ushauri sahihi au tiba pia juu ya tatizo lako.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!