Connect with us

Magonjwa

UGONJWA WA RED EYES(chanzo,dalili,madhara na tiba)

Avatar photo

Published

on

RED EYES

UGONJWA WA RED EYES(chanzo,dalili,madhara na tiba)

Ugonjwa wa red eyes ni ugonjwa ambao huhusisha macho kuwa mekundu kama dalili kubwa.

CHANZO CHA UGONJWA WA RED EYES

Ugonjwa wa Red eyes hutokana na mashambulizi ya vimelea vya magonjwa kama vile Virusi ambao husababisha vishipa vidogo ndani ya macho kuvimba na kupasuka, kisha damu kuvilia ndani ya jicho.

DALILI ZA UGONJWA WA RED EYES NI PAMOJA NA;

• Macho kubadilika rangi na kuwa mekundu

• Kuwashwa na macho

• Kuhisi kitu kama mchanga ndani ya jicho lako

• Kuvimba macho yako

• N.K

MATIBABU YA UGONJWA WA RED EYES

– Ugonjwa huu hupona wenyewe ndani ya siku 3 mpaka 5 kulingana na uwezo au uimara wa kinga yako ya mwili Wala huhitaji matumizi ya dawa yoyote ile.

Japo lazima kwanza kuchuguzwa na wataalam wa afya baada ya kujihakikishia kuwa ni shida ya red eyes watakupa maelekezo kwa kina ikiwa ni pamoja na jinsi ya kutunza jicho lako.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LILE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA MACHO MEKUNDU (RED EYES)

✅ Maambukizi ya kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho yajulikanayo kitaalam “Viral Keratoconjunctivitis” ni Maambukizi yanayosambaa kwa kasi kubwa .Hakuna tiba maalum kwa ugonjwa huu na hata bila tiba, dalili huisha zenyewe ndani ya wiki mbili . Usafi ni jambo muhimu katika kuzuia maambukizi haya kusambaa kwa wengine.

✅ Mlipuko huu husababishwa na Kirusi kijulikanacho kwa jina la “Adenovirus”kwa zaidi ya asilimia 80%.

JINSI YA KUZUIA UGONJWA WA MACHO MEKUNDU.

✅Watoto wadogo Wagonjwa wanaoenda shule wanashauriwa wanashauriwa wakae nyumbani hadi dalili zinapoisha kwa kuwa ni ngumu kuzuia maambukizi yasisambae kwenye mazingira ya shule.

✅Watu wazima wanaweza kwenda kazini ila wanapaswa kuzingatia kanuni za kuzuia kutokuambukizwa au kuambukiza wengine kwa kufuata kanuni za kuzuia maambukizi.

✅ Watumishi wa Afya wazingatie kutopeleka Maambukizi hayo nyumbani kwa kufuata kanuni za kuzuia maambukizi.

Red Eyes: au kwa jina lingine “Macho mekundu” ni neno linalotumika kuelezea macho yaliyopata wekundu, kuwasha, na kuwa na viashiria vya damu (bloodshot). Wekundu huu hutokea pindi vimishipa midogo ya damu chini ya uso wa jicho vinapotanuka au kuvimba. Mara nyingi, ni athari ya ukereketaji (irritation) au mashambulizi (infection) ya kwenye jicho.

Macho mekundu yanaweza kuathiri jicho moja au yote mawili. Pia ni hali ambayo inaweza kutokea taratibu au kwa ghafla, kama vile kwa matatizo ya mzio au jeraha la jicho.

Unaweza kuwa na macho mekundu na dalili nyingine kama vile:

  • Maumivu ya jicho.
  • Kuwasha.
  • Kutokwa na matongotongo.
  • Kuvimba kwa jicho.
  • Mabadiliko katika kuona, kama vile kuona ukungu.

Hatua na viwango tofauti vya ukali wa macho mekundu

Mara nyingi, macho mekundu athari zake huwa kubwa kwa muonekano kuliko jinsi unavyojisikia ndiyo maana kwa wengi huwa hawahisi kitu mpaka wanapoenda kujiangalia na kugundua kuwa jicho limekuwa jekundu. Katika visa vingi, macho mekundu ni ya kawaida na mara nyingi hutibiwa na matibabu ya nyumbani au matibabu ya madawa ya kawaida (OTC).

Lakini ikiwa jicho lako au macho yako yanaendelea kuwa mekundu kwa zaidi ya wiki moja, au una maumivu au matatizo kwenye kuona, hakikisha unaweka miadi ya kuonana na daktari haraka uwezavyo, unaweza kuonana na daktari wa macho ophthalmologist (eye doctor) au daktari wa miwani optometrist.

Ni nini chanzo cha kawaida cha macho mekundu?

Kuna sababu nyingi zinazoweza kupelekea kupata tatizo la macho mekundu, macho yanaweza kupata wekundu kutokana na uvaaji wa lenzi za kuweka machoni kwa muda mrefu au umekaa kwenye kompyuta kwa muda mrefu bila kupata mapumziko. Baadhi ya sababu nyingine za kawaida ni pamoja na:

  • Mzio (Allergies).
  • Tatizo la Blepharitis.
  • Maambukizi kwenye ngozi ya juu ya gololi (Viral Keratoconjunctivitis).
  • Jicho kavu.
  • Jeraha la jicho.
  • Ugonjwa wa Glakoma (Glaucoma).

Mambukizi ya kirusi kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho yajulikanayo kitaalamu “Viral Keratoconjunctivitis”

Haya ni moja ya maambukizi ambayo hulipuka sana kwenye jamii zetu, Mambukizi ya kirusi kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho yajulikanayo kitaalamu “Viral Keratoconjunctivitis”, ni maambukizi yanayosambaa kwa kasi kubwa. Hakuna tiba maalumu kwa ugonjwa huu na hata bila tiba, dalili huisha zenyewe ndani ya wiki mbili. Usafi ni jambo muhimu kuzuia maambukizi haya kusambaa kwa watu wengine.  Mlipuko huu husababishwa na Kirusi kijulikanacho kwa jina la Adenovirus kwa asilimia zaidi ya 80%.

Dalili huonekana kuanzia siku 5 hadi 14 baada ya kupata vimelea vya maambukizi. Aidha, mara chache inaweza kuchukua muda mrefu zaidi. Pia, mtu huchukua siku 1 hadi 2 mpaka kuanza kuonesha dalili na anaweza kuendelea kuambukiza takriban wiki mbili baada ya dalili kuanza kuonekana.

Hadi sasa hakuna tiba maalumu kwa maambukizi ya ugonjwa huu, na dalili huisha kwa muda wa wiki 2, wakati mwingine zinaweza kuendelea kwa wiki hadi 6. Wagonjwa wanashauriwa kufika kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kwa ajili ya kupimwa na kupatiwa dawa za kupunguza madhara kulingana na ishara zitakazoonwa na Daktari.

Maambukizi haya husambazwa kwa njia zifuatazo;

Kugusa machozi au matongotongo kutoka kwenye macho ya mtu mwenye maambukizi.

Kugusana mikono na mtu mwenye maambukizi halafu ukajishika machoni.

Macho Mekundu Yanaonekanaje na Kujisikiaje?

Wakati mwingine, jicho lako linaweza kuwa jekundu mahali ambapo palipaswa kuwa kweupe. Hii inaweza kutokea pindi vimishipa vya damu vilivyopo ndani ya macho yako vimevimba kuliosababishwa na kukereketa kwa jicho. Pia, inawezekana kabisa kuwa vimishipa vidogo vidogo vimepasuka.

Ikiwa jicho lako limekuwa jekundu kutokana na jeraha, basi inawezekana kuwa jicho limefungua zaidi (dilate) vimishipa vya damu katika jicho lako ili kuruhusu damu zaidi kufika kwenye eneo hilo kwa ajili ya kuharakisha uponyaji kwani damu ndiyo nyezo inayotumika kwenye uponyaji ndani ya mwili wa binadamu. ufungukaji mkubwa wa vimishipa hivi ndiyo inayosababisha macho kuwa mekundu.

Kulingana na hali inavyoendelea, macho yako mekundu yanaweza kujisikia:

Halina shida yoyote, kwa wengi wenye hali hii hawawezi kujua kama wana jicho jekundu mpaka wajiangalie au waambiwe na watu wengine.

Kuwasha au kuwa na kero, mara nyingi kwa wale walipata maambukizi (infection).

Jinsi ya kujisaidia

Kumbuka kuwa, kuna aina nyingi sana za macho mekundu, baadhi yake unaweza kujitibia wewe mwenyewe nyumbani na nyingine utajitaji msaada wa haraka wa daktari.

✓ Pata mapumziko ya kutosha.

✓ Weka kitambaa kizito juu ya macho yaliyofungwa.

✓ Fanyia massage ngozi ya juu ya jicho (eyelid)

✓ Kwa utaratibu kabisa safisha ngozi ya jicho (eyelid) kwa kutumia maji safi.

✓ Unaweza kuweka matone ya dawa za kawaida (OTC).

✓ Wakati mwingine, mtaalam wa huduma ya macho anaweza kupendekeza na kutoa dawa za viua vijasumu (antibiotics), matone maalum ya macho, au dawa za kunywa.

Ni nini hatari au madhara yanayowezekana ikiwa macho mekundu hayatibiwi?

Kwa mara nyingi, macho mekundu si hatari na inaweza hata isiwe na haja ya matibabu. Hata hivyo, kuna hali zinaweza kuwa na athari kubwa zaidi na zitakuladhimu upate matibabu ya kina.

Ikiwa umekaa na jicho jekundu kwa zaidi ya siku moja au mbili, au ikiwa tatizo hili limempata mtoto mdogo, basi unashauriwa uwasiliane na mtoa huduma za afya kwa uangalizi zaidi.

Pia, unatakiwa kuwasiliana na mtoa huduma pindi unaposikia maumivu au jicho linatoa matongotongo au uchafu wowote.

Endapo jicho lako kuwa jekundu ni matokeo ya athari kubwa kwenye jicho, endapo utakaa nalo bila ya matibabu linaweza kupelekea matatizo makubwa ikiwemo kupoteza uwezo wa kuona.

Jinsi ya kuepuka macho mekundu.

Si rahisi kuepuka kila macho mekundu, lakini unaweza kupunguza uwezekano wa kupata macho mekundu kwa kufuata ushauri ufuatao;

Usipendelee kusugua macho kwa kutumia mkono. Uchafu na vijidudu (germs) vilivyopo kwenye mikono yako vinaweza kusababisha madhara makubwa zaidi ya jicho kuwa jekundu au kukereketa (irritation).

Kama unatumia lenzi za ndani ya macho, hakikisha ni safi na usiweke kupitiliza muda ulioshauriwa.

Kwa wadada, tumia njia sahihi kuondoa urembo (make up) na hakikisha macho yako yanabaki masafi.

Hakikisha unapata muda wa kupumzika kila utumiapo kompyuta. Usitumie kwa muda mrefu bila kupata mapumziko.

Epuka vitu vinavyoweza kupelekea jicho kukereketa kama vumbi,moshi nk.

Hakikisha unajenga desturi ya kunawa mikono kwa maji safi na yanayotiririka kwa sabuni mara kwa mara kuzuia kupata maambukizi.

Onana na daktari pindi unapoona unapata macho mekundu mara kwa mara au umepata macho mekundu yasiyoisha.

Usichangie vipodozi na vitu vingine unavyotumia kama vile taulo za karatasi au nguo au dawa za macho.

Funika mdogo na pua wakati wa kukohoa au kupiga chafya ili kuzuia kuambukiza wengine.

Dalili za hatari

Ingawa macho mekundu huisha yenyewe baada ya muda, ila kuna wakati, macho mekundu ni ishara ya ugonjwa mkubwa.Wasiliana na daktari pindi unapoona;

Jicho linauma.

Umeanza kuwa na uono hafifu.

Macho yanakuwa yanaogopa mwanga kupitiliza (extra sensitive to light).

Una dalili zaidi ya wiki na zimekuwa zikiendelea kuwa mbaya.

Jicho limekuwa likitoa matongotongo yanayoganda kwenye kope.

Umepata homa au maumivu yanayoambatana na kujisikia vibaya.

Hakikisha unaenda hospitari haraka iwezekanavyo pindi unapoona moja ya dalili hizi;

– Jicho linauma kupitiliza.

– Unaogopa mwanga kupitiliza.

– Jicho limevimba.

– Unaona ukungu.

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In https://afyaclass.com Also Follow us on Instagram @afyaclass

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa3 months ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa3 months ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa3 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa3 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa5 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake5 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa4 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa2 days ago

kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani

kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani Unapopata tatizo la kuharisha na kutapika kwa wakati mmoja unaweza kuwaza sana,...

Magonjwa4 days ago

Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu

Dalili za infection kwenye damu Mchafuko wa damu,chanzo,dalili na Tiba Mchafuko wa damu; hiki ni kiswahili ambacho watu wamezoea kukitumia...

Magonjwa1 week ago

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri Yapo magonjwa mbali mbali ya ngozi ambayo huweza kuathiri Sehemu za Siri za Mwanaume...

Magonjwa2 weeks ago

Dalili za acid reflux,Soma hapa Kufahamu

Dalili za acid reflux: Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD), ni tatizo ambalo huwapata Watu wengi,Tatizo hili hujulikana kwa jina...

Magonjwa4 weeks ago

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe au ni ugonjwa ambao huhusisha ngozi kupoteza rangi...

Magonjwa4 weeks ago

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu Baada ya Ugonjwa huu wa macho kusumbua watu wengi kwa kipindi cha Hivi Karibuni,...

Magonjwa1 month ago

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu Utangulizi: Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo...

Magonjwa1 month ago

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume Gono ni neno maarufu ambalo kirefu chake ni Gonorrhea na kiswahili chake ni...

Magonjwa1 month ago

Dalili Mpya za ukimwi kwenye ngozi

Zipi ni Dalili za ukimwi kwenye ngozi Zipi ni dalili za Ukimwi kwenye ngozi ya mtu? Fahamu hapa kupitia makala...

Magonjwa1 month ago

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu Huu ni ugonjwa wa kuambukiza uliosababishwa na kirusi cha corona, ambao...

Trending