MIGUU
• • • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA KUPASUKA MIGUU KWENYE KISIGINO(gaga)
Tatizo la kupasuka miguu kwenye visigino maarufu kama magaga, ni tatizo ambalo huwapata watu wengi na wengine hadi kufikia hatua ya kupata maumivu makali sana, damu kutoka n.k
CHANZO CHA TATIZO LA KUPASUKA MIGUU KWENYE KISIGINO(gaga)
- Ngozi ya miguuni kwenye Visigino kukauka kupita kiasi huweza kuchangia hali ya mpasuko kwenye visigino vya miguuni
- Kutokana na presha kubwa au mgandamizo wa sehemu ya chini ya miguuni ambayo hubeba mwili mzima hasa wakati ukiwa umesimama husababisha ngozi ya kwenye kisigino kuvutika kupita kiasi hivo kupelekea kupasuka
- Maambukizi ya Fangasi wa miguuni yaani athlete's foot huweza kuwa chanzo kingine cha tatizo hili
WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA SHIDA HII YA KUPASUKA KWENYE KISIGINO
✓ Wanaopenda kutembea chini bila viatu mara kwa mara
✓ Wenye shida ya fangasi wa miguuni
✓ Ambao hawanywi maji ya kutosha kila siku
✓ Wanaokaa maeneo yenye baridi sana
✓ Ambao hawaoshi miguu yao mara kwa mara
✓ Wanaopenda kuoga na maji ya moto sana au kuweka miguu kwenye maji ya moto kwa muda mrefu
✓ Wenye ugonjwa wa Kisukari
✓ Wanaopenda kusugua miguu hasa ikiwa mikavu
✓ Wanene kupita kiasi au wenye tatizo la Uzito mkubwa
✓ Wanaofanya kazi za kusimama muda mrefu
✓ Wenye shida ya Eczema
✓ Na wenye matatizo mengine kama vile;
• Kuwa na kiwango kidogo cha hormones au vichocheo vya Thyroid hali ambayo hujulikana kama Hypothyroidism
• Juvenile Plantar dermatosis
• Flat feet
N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!