FAHAMU KUHUSU BACTERIA ANAYESABABISHA VIDONDA VYA TUMBO Maarufu kama Helicobacter Pylori

 HELICOBACTER PYLORI

• • • • • •

FAHAMU KUHUSU BACTERIA ANAYESABABISHA VIDONDA VYA TUMBO Maarufu kama Helicobacter Pylori


Helicobacter Pylori ni Bacteria ambaye huweza kusababisha matatizo mbali mbali kwenye mwili wa Binadamu ikiwa ni pamoja na tatizo la Vidonda vya Tumbo au Peptic Ulcers.


Maambukizi ya Bacteria HELICOBACTER PYLORI huweza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia njia ya Mate,matapishi,Kinyesi n.k


DALILI ZA MAAMBUKIZI YA HELICOBACTER PYLORI


- Bacteria huyu huanza kushambulia watoto wadogo na Watu wengi hawaonyeshi dalili yoyote baada ya maambukizi,


Dalili za Maambukizi ya H.Pylori ni pamoja na;


• Mtu kupata maumivu makali ya tumbo hasa akiwa na Njaa


•  Kuhisi hali ya kuungua tumboni


• Kuhisi kichefuchefu na kutapika mara kwa mara


• Hamu ya chakula kupotea


• Tumbo kujaa gesi mara kwa mara


• Uzito wa mwili kupungua kwa kasi

N.k


UKIWA NA DALILI HIZI HAPA UNATAKIWA KUPATA TIBA MAPEMA


✓ Maumivu makali sana ya tumbo mpaka unashindwa kufanya chochote au mwili kukosa nguvu


✓ Kushindwa kumeza kitu chochote


✓ Kujisaidia kinyesi kimechanganyika na Damu


✓ Kutapika matapishi ambayo yamechanganyika na Damu


MADHARA YA MASHAMBULIZI YA HELICOBACTER PYLORI


~ Mtu kupata vidonda vya tumbo au Peptic Ulcers


~ Kuvimba kwa kuta za tumboni


~ Kupata Kansa ya tumbo


MATIBABU YA MASHAMBULIZI YA HELICOBACTER PYLORI


• Tatizo hili hutibiwa kwa Dawa mbali mbali kama vile;


- Dawa jamii ya PROTON PUMP INHIBITORS ambazo huzuia uzalishaji wa Acid tumboni kama vile; OMEPRAZOLE, ESOMEPRAZOLE, PANTOPRAZOLE n.k


- Dawa jamii ya HISTAMINE BLOCKERS kama CIMETIDINE n.k


Kujua zaidi Kuhusu VIDONDA VYA TUMBO soma hapa


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!