Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU KWA KINA KUHUSU CD4 NA FAIDA ZAKE MWILINI



 CD4

• • • • •

FAHAMU KWA KINA KUHUSU CD4 NA FAIDA ZAKE MWILINI


Bila shaka sio Mgeni kuhusu kusikia kitu kinaitwa CD4, Lakini hufahamu kwa kina CD4 ni kitu gani na faida zake ni zipi. Soma hapa kujua zaidi..!!!


CD4 NI NINI?


CD4 ni kifupi cha maneno haya "Cluster of differentiation 4" ambapo maana yake halisi, tunazungumzia kuhusu Aina ya Glycoprotein ambayo hupatikana kwenye seli za kinga ya mwili au kwa lugha nyingine seli nyeupe za damu(WHITE BLOOD CELLS),


Kama vile; T-helper cells, monocytes, macrophages, Dendritic cells n.k


CD4 zimegundulika miaka ya 1970 ambapo zilikuwa zinajulikana kama Leu-3 na T4 ndani ya mwili wa binadamu kama ilivyokuwa inajulikana sana ndani ya miaka ya 1984


FAIDA YA CD4 MWILINI


CD4 cells ni sehemu ya white Blood cells ambazo kazi yake kubwa ni kuhakikisha Kinga ya mwili Inaimarika yaani Health body immune system na kusaidia kuukinga mwili dhidi ya magonjwa mbali mbali


JE UNATAKIWA UWE NA SELI ZA CD4 KIASI GANI MWILINI?(CD4 COUNT)


- Kwa mtu ambaye ana afya njema anatakiwa awe na CD4 seli kuanzia 500 mpaka 1,400 per Cubic millimeter za damu


- Kuwa na kiwango cha chini ya seli 200  per cubic millimeter za damu upo kwenye hatari ya kushambuliwa na magonjwa mbali mbali mwilini,kwani mwili wako utakuwa hauna kinga ya kutosha ya kupambana na magonjwa mbali mbali.


KUMBUKA;


✓ Kwa mtu ambaye ana maambukizi ya virusi vya UKIMWI kama hatumii dawa yaani ART, seli hizi huendelea kupungua kwa kiwango kikubwa sana, na kumuweka kwenye hatari ya kushambuliwa na kila aina ya ugonjwa


✓ CD4 count huweza kushuka chinu kutokana na sababu mbali mbali kama vile;


• Maambukizi ya magonjwa kama HIV


• Matumizi ya baadhi ya dawa

N.k


NA tatizo la LEUKOPENIA hupunguza CD4 count lakini kwa tatizo kama LEUKOCYTOSIS huongeza sana CD4 count.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments