Ticker

6/recent/ticker-posts

KANSA YA MFUPA,chanzo cha Saratani Hii,Dalili Na TIBA



 BONE CANCER

• • • • • •

KANSA YA MFUPA,chanzo cha Saratani Hii,Dalili Na TIBA


Aina hii ya kansa huathiri mfupa wowote mwilini ingawa kwa asilimia kubwa hushambulia mfupa wa kiunoni yaani PELVIC Bone pamoja na mifupa mirefu kama ya Mikono na Miguu.


DALILI ZA KANSA YA MFUPA ni pamoja na;


- Mtu kupata maumivu makali ya Mfupa


- Kuvimba eneo ambalo limeathiriwa


- Ngozi ya eneo ambalo limeathiriwa kubadilika rangi na kuwa jekundu


- Mfupa kuwa dhaifu zaidi na kuvunjika kwa haraka zaidi


- Mwili kuchoka kupita kawaida


- Uzito wa mwili kushuka kwa kasi zaidi

n.k


CHANZO CHA KANSA YA MFUPA


• Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo huhusishwa na aina hii ya Kansa, japo tafiti zinaonyesha kwamba kuna baadhi ya sababu ambazo huongeza uwezekano wa kutokea kwa shida hii ya Saratani au Kansa ya Mfupa na sababu hizo ni kama vile;


✓ Kurithi vina saba vya tatizo hili katika familia


✓ Mtu kupata huduma ya mionzi mara kwa mara hapo kabla ya kuumwa


✓ Kuwa na magonjwa ya mifupa kama vile; Paget's disease


✓ Umri kuwa mkubwa zaidi


MATIBABU YA KANSA HII YA MFUPA


- Matibabu ya kansa ya Mfupa hutegemea na aina, stage ya kansa, pamoja na hali ya Mgonjwa,


Kwa ujumla wake matibabu ya Kansa ya mfupa ni kama vile;


✓ Upasuaji


✓ Huduma ya mionzi yaani Radiotherapy


✓ Chemotherapy


✓ Matumizi ya dawa mbali mbali ikiwemo za maumivu

N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments