Ticker

6/recent/ticker-posts

KITU AMBACHO HUKIJUI KUHUSU UPIMAJI WA VIRUSI VYA UKIMWI(Golden test)



  UKIMWI

• • • • •

KITU AMBACHO HUKIJUI KUHUSU UPIMAJI WA VIRUSI VYA UKIMWI(Golden test)


Fahamu kwamba upimaji wa virusi vya Ukimwi huhusisha hatua Kuu Mbili, na hatua hizi mbili huhusisha vipimo viwili Tofauti, 


UPIMAJI HATUA YA KWANZA


- Upimaji hatua ya kwanza huhusisha kipimo ambacho hujulikana kama RAPID TEST,


ambapo mtu hupimwa kwa mara ya kwanza afikapo Hospitalini au kituo chochote cha afya,


ENDAPO; majibu ni NEGATIVE, basi mtu huyu hushauriwa kurudi baada ya Kipindi cha MIEZI 3 ili kurudia vipimo, kwani maambukizi mapya huonekana baada ya miezi 3 kwa asilimia 98% ya Wagonjwa


ENDAPO; majibu ni POSTIVE kwa kipimo cha Kwanza yaani Rapid Test, Basi mtu huyu huingia hatua ya Pili ya vipimo


UPIMAJI HATUA YA PILI


- Baada ya kipimo cha kwanza(Rapid test) kuonyesha kwamba mtu ni POSITIVE, basi huingia vipimo hatua ya pili


- Vipimo hatua ya pili huhusisha kipimo kinachojulikana kama GOLDEN TEST,


Endapo kipimo hiki kikionyesha POSITIVE tena, basi moja kwa moja mtu huyu ni Muathirika wa Virusi vya Ukimwi


KUMBUKA; Huwezi kusema mtu ni muathirika wa virusi vya ukimwi kwa kipimo kimoja cha Awali, lazima uingie kwenye Confirmatory TEST yaani Golden Test.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments