Ticker

6/recent/ticker-posts

MACHO KUTOA MACHOZI YENYEWE(chanzo cha tatizo hili na Tiba yake)



   MACHO

• • • • • 

MACHO KUTOA MACHOZI YENYEWE(chanzo cha tatizo hili na Tiba yake)


Baadhi ya watu hupatwa na tatizo hili la macho kutoa machozi yenyewe ambapo huweza kuwa jicho moja au yote mawili. chanzo chake ni nini?


CHANZO CHA TATIZO LA MACHO KUTOA MACHOZI YENYEWE


Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia tatizo hili kama vile;


- Tatizo la allergy au mzio ambayo huweza kupata macho yako juu ya vitu flani kama vile; vumbi,perfumes,mafuta n.k


- Kuvimba kwa kuta za ndani ya jicho yaani kwa kitaalam Inflammation under eye surfaces


- Macho kuwasha kutokana na baadhi ya vitu kuingia jichoni


- Macho kuwa makavu kupita kawaida hali ambayo hupelekea kuzalishwa kwa machozi kupita kawaida ndani ya jicho ili kuondoa tatizo la ukavu machoni


- Kuziba kwa baadhi ya vimirija vidogo sana machoni hali ambayo huathiri ukaushwaji wa machozi yakizalishwa yaani poor eyes drainage system


- Kuingiwa na kitu chochote jichoni kama vile; mdudu,mchanga n.k


- Tatizo la Tezi aina ya oil gland ndani ya jicho


- Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kwenye jicho kama vile; Bacteria,Fangasi au Virusi


- Na matatizo mengine kama vile; Bell's palsy n.k


MATIBABU YA TATIZO HILI LA MACHO KUTOA MACHOZI YENYEWE


• Matibabu ya tatizo hili la macho kutoa machozi yenyewe hutegemea na chanzo chake, hivo kama nilivyotaja vyanzo mbali mbali vya tatizo hili hapo juu,


Ili kujua chanzo na kupata tiba sahihi ya tatizo lako,ni vizuri kukutana na wataalam wa Afya ya Macho


AU


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments