MADHARA YA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB)

  KIFUA KIKUU

• • • • •

MADHARA YA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB)


Ugonjwa wa kifua kikuu maarufu kama TB au Tuberculosis ni ugonjwa ambao husababishwa na Bacteria anayejulikana kwa jina la mycobacterium Tuberculosis


Bacteria huyu husambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia vitone vidogo vidogo kwenye hewa baada ya mgonjwa kukohoa au kupiga chafya.


DALILI ZA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;


- Mgonjwa kukohoa kwa wiki 3-4


- Mgonjwa kukohoa damu au maji maji,usaha n.k


- Mgonjwa kupata maumivu makali ya kifua


- Mgonjwa kupata shida ya upumuaji


- Mgonjwa kuchoka sana


- Uzito wa mwili kushuka kwa kasi


- Mgonjwa kutoa sana jasho wakati wa usiku


- Mgonjwa kupata homa za mara kwa mara

n.k


MADHARA YA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB)


• Ugonjwa wa kifua kikuu au TB huweza kusababisha maumivu makali ya Mgongo


• Ugonjwa wa kifua kikuu au TB huweza kusababisha kuharibika kwa joints


• Ugonjwa wa kifua kikuu au TB huweza kusababisha kuvimba kwa ngozi inayofunika ubongo hali ambayo hujulikana kama MENINGITIS


• Ugonjwa wa kifua kikuu au TB huweza kusababisha matatizo ya ini


• Ugonjwa wa kifua kikuu au TB huweza kusababisha matatizo ya Figo


• MARA CHACHE PIA, Ugonjwa wa kifua kikuu au TB huweza kusababisha matatizo ya moyo


WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA KIFUA KIKUU AU TB


✓ Wagonjwa wa UKIMWI


✓ Wagonjwa wa KISUKARI


✓ Wenye magonjwa ya Figo


✓ Wenye tatizo la KANSA


✓ Wanaopatiwa huduma na matibabu ya Kansa kama vile CHEMOTHERAPY


✓ Wanaotumia dawa za kuzuia ORGAN TRANSPLANT REJECTION


✓ Wenye shida ya Utapiamlo


✓ Wafanyakazi wa Afya wanaohudumia wagonjwa wa kifua kikuu au TB


✓ Wanaotumia Tumbaku

N.K



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!