SARATANI YA UUME(dalili zake na Watu waliopo kwenye hatari ya kupata)
AFYA YA UZAZI
• • • • • •
SARATANI YA UUME(dalili zake na Watu waliopo kwenye hatari ya kupata)
Kumekua na ongezeko la visa vya wanaume kupata saratani ya uume barani afrika na hata Tanzania pia. Saratani ya uume inaleta madhara makubwa sana kwa mwili ikiwemo kupoteza kujiamini au kujithamini kwa mwanaume na hata kupoteza maisha ya mwanaume kinachosababisha saratani ya uume kwa kweli hakijulikani lakini ziko baadhi ya sababu ambazo zimeonekana kuchangia kama nitakavoelezea hapo chini.
WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA SARATANI YA UUME
1)Wanaume ambao hawajatahiriwa
2)Maambukizi ya HPV
3)Wanaume wenye UKIMWI
4)Wanaume wanaovuta sigara
5)Matumizi ya tumbaku na uvutaji sigara
6)Uchafu
7)Maambukizi kwenye kichwa cha uume
8)Magonjwa ya zinaa
9) Ugonjwa wa likeni
DALILI
Dalili kuu ya kuwepo kwa saratani ya uume ni mabadiliko ya ngozi ya uume kwa maana ya kua nyeusi sana,ngumu sana,kuota vinundu au vipele vigumu hasa hasa kwenye kichwa cha uume,kua na vidonda vya muda mrefu ambavyo haviumi
VIPIMO NA MATIBABU
Saratani hii kama ilivo saratani zingine kama ukiiwahi kuigundua na kuitibu basi matokeo hua mazuri sana na uwezekano wa kubaki na uume wako utakua mkubwa. Kama unaona una mabadiliko yeyote kwenye uume wako basi fika hospitali ili uchekiwe na upate tiba stahiki. Baadhi ya vipimo vya kufanyiwa ni kukitazama kwa mikono,kuchukua kinyama kwa ajili ya kukipima,kufanya vipimo kama CT scan au MRI ili kuona ukubwa wa tatizo.
Matibabu ya saratani hii hutegemea na hatua za ugonjwa ulikofikia,kama ukiwahi basi unaweza kupewa dawa za mishipa,mionzi,kuvichoma vivimbe kwa baridi. Kama ukija saratani ikiwa imeshasambaa basi tiba inakua ni KUKATA HUO UUME ili kukufanya uishi vizuri na kuokoa maisha yako
Cr:Dr.Mathew
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!