MWILI
• • • • •
TATIZO LA KUWASHWA MWILI mara baada ya Kuoga CHANZO na Tiba
Baadhi ya watu hupatwa na tatizo la Ngozi kuwasha mara tu baada ya Kuoga, Je chanzo chake ni nini?, Je ni hali ya kawaida au tatizo? soma hapa kujua.
Sio kila mtu ambaye hupatwa na miwasho mara tu baada ya kuoga ni hali ya kawaida, Soma hapa katika makala hii kujua baadhi ya sababu ambazo huweza kuchangia tatizo la mtu kuwashwa baada ya Kuoga.
SABABU ZA MTU KUWASHWA MWILI BAADA YA KUOGA
- Tatizo la Allergy au kwa kiswahili hujulikana kama Mzio, mtu huweza kuwa na allergy na baadhi ya vitu kama vile; Sabuni, maji n.k hali ambayo huweza kusababisha tatizo hili la kuwashwa baada ya kuoga.
- Tatizo la fangasi wa ngozi pamoja na kwenye Damu,
Pia fangasi huweza kuchangia kwa kiasi kikubwa mtu kupatwa na tatizo la kuwashwa na ngozi mara kwa mara
- matumizi ya baadhi ya dawa za kufanyia usafi bafuni,chooni N.k ambazo huwa na kemikali zenye viambata vya sumu ambazo huweza kuleta shida ya kuwashwa kwenye ngozi
- mtu kupatwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi au damu,huweza pia kuchangia uwepo wa tatizo hili
- Kinga ya mwili kushuka kupita kawaida
- Magonjwa ya Figo, kisukari,Ini pamoja na nyongo
- Kuwa na tatizo la ngozi kukauka kupita kawaida
- magonjwa mbali mbali ya zinaa huweza kusababisha miwasho hasa sehemu za siri
- magonjwa ya mfumo wa fahamu au kwa kitaalam nerves
- matatizo ya akili
N.k
MATIBABU YA TATIZO HILI
- tiba ya tatizo hili huanzia na chanzo chake, kama nilivyokwisha kuelezea baadhi ya vyako vyake hapo juu,
Mfano kama tatizo ni allergy basi mgonjwa huweza kupewa dawa mbali mbali kama vile; CETRIZINE,ERTHROMYCIN n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!