Tatizo la mtoto kuchemka au Kuwa na homa

 HOMA

• • • • • •

Tatizo la mtoto kuchemka au kuwa na homa


Joto la mtoto huweza kuwa juu sana au mtoto kuwa na homa na wengine hutumia kiswahili cha mtoto kuchemka. Hali hii ni pale ambapo joto la mtoto ni kuanzia nyuzi joto 38 na kuendelea.


wataalam wa afya hushauri mtoto kupimwa joto lake la mwili mara kwa mara ili kujua joto lake halisi akiwa katika hali yake ya kawaida,


SABABU ZA JOTO LA MTOTO KUWA JUU


Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia joto la mtoto kuwa juu kama vile;


1. Mtoto kuwa na tatizo la upungufu wa maji ya mwili


2. Mtoto kuvalishwa nguo nyingi na nzito wakati wa joto,


Inashauriwa kwamba mtoto hutakiwa kuvaa nguo mara mbili zaidi yako ulivyovyaa kulingana na hali ya mazingira ilivyo,


mfano; Kama wewe ukivaa nguo tatu kutokana na hali ya hewa ilivyo unajisikia vizuri,basi mtoto mvalishe nguo nne, kama wewe umevaa mbili yeye avae tatu, kama wewe umevaa mbili basi yeye avae tatu.


3. Joto la mtoto huweza kuwa juu tokana na maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria,Virusi n.k


4. N.k


Hata hivo tatizo la mtoto kuwa na homa katika umri mdogo sana sio dalili nzuri, hivo mtoto huyu huhitaji uchunguzi wa kina kutoka kwa wataalam wa afya


✓ FAHAMU; Mwili kupandisha joto kukiwa na mashambulizi ya magonjwa husaidia mwili kupambana na maambukizi hayo pamoja na kuwa rahisi sana kwa Bacteria au Virusi ambao hawapendi mazingira ya joto kuharibiwa na Mfumo wa kinga ya mwili wako.


KWA USHAURI  ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA  +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!