TATIZO LA UKE KUWA MWEMBAMBA,KUKAUKA NA KUVIMBA(vaginal atrophy)

  VAGINAL ATROPHY

• • • • •

TATIZO LA UKE KUWA MWEMBAMBA,KUKAUKA NA KUVIMBA(vaginal atrophy)


Vaginal atrophy hili ni tatizo ambalo huhusisha uke wa mwanamke kuwa mwembamba,kukauka pamoja na kuvimba


Wanawake wengi hupata hili tatizo baada ya kufikia kipindi cha ukomo wa hedhi yaani Menopause


CHANZO CHA TATIZO HILI


Tatizo hili hutokana na Uwepo wa kiwango kidogo cha ESTROGEN mwilini kutokana na sababu mbali mbali kama vile;


- Baada ya mwanamke kufikia ukomo wa hedhi


- Baada ya upasuaji wa kuondoa Ovary zote mbili


- Baada ya matumizi ya dawa ambazo huathiri uzalishaji wa kichocheo cha Estrogen kama baadhi ya dawa za kupanga uzazi


- Baada ya kupata huduma ya mionzi kwa ajili ya matibabu ya kansa hasa Pelvic Radiation


- Huduma ya Chemotherapy

N.k


DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


• Mwanamke kuwa mkavu ukeni


• Kuhisi hali ya kuungua ukeni


• Kutokwa na uchafu ukeni


• Kuwashwa sehemu za siri


• Kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa


• Kukojoa mara kwa mara


• Kupata maambukizi ya ugonjwa wa UTI ambayo hujirudia rudia mara kwa mara


• Mwanamke kushindwa kuzuia mkojo kutoka yaani Urinary Incotinence


• Kutokwa na damu kidogo yaani Light bleeding wakati wa kufanya tendo la ndoa


• Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa


• N.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


- Zipo njia mbali mbali za kutibu tatizo hili kama vile; Matumizi ya dawa za kuongeza kiwango cha ESTROGEN mwilini mfano;


✓ Vaginal Estrogen Suppositories


✓ Vaginal Estrogen Cream

N.k



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!