Ugonjwa wa Kuvimba kwa Ini,Chanzo,dalili na Tiba yake

 INI

• • • • •

Ugonjwa wa Kuvimba kwa Ini,Chanzo,dalili na Tiba yake


Ini ni miongoni mwa viungo ambavyo hufanya kazi nyingi kuliko viungo vingine mwilini, Katika makala hii tunazungumzia matatizo ambayo huweza kukumba Ini lako ikiwa ni pamoja na tatizo la kuvimba kwa Ini.


CHANZO CHA KUVIMBA KWA INI PAMOJA NA MATATIZO MENGINE YA INI


- Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa ikiwa ni Pamoja na mashambulizi ya VIRUSI kama vile; Hepatitis Virus A,B,C n.k


- Matatizo katika mfumo wa kinga ya mwili kama vile;Primary Biliary Cholangitis, Autoimmune hepatitis n.k


- Matatizo ya kigenetics kama vile; Wilson's disease, Hemochromatosis n.k


- Aina mbali mbali za kansa au Saratani kama vile; Saratani ya Ini, Saratani ya mrija wa nyongo yaani Bile duct cancer n.k


- Matumizi ya pombe kupita kiasi


- Mafuta kujikusanya kwa kiwango kikubwa kwenye Ini kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ya Unene kupita kawaida

N.k


DALILI ZA  KUVIMBA KWA INI PAMOJA NA MATATIZO MENGINE YA INI NI PAMOJA NA;


1. Macho pamoja na ngozi ya mwili kubadilika rangi na kuwa manjano ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Jaundice


2. Kuwa na tatizo la kuvimba miguu


3. Kuwa na tatizo la kuwashwa mwilini


4. Kukojoa mkojo wenye rangi nyeusi


5. Kujisaidia kinyesi ambacho hakina rangi yake ya kawaida au tunasema pale stool color


6. Kupata uchovu wa mwili ambao hauishi


7. Kukosa kabsa hamu ya chakula


8. Kuwa na tatizo la kichefuchefu pamoja na Kutapika

N.K


MATIBABU YA MATATIZO YA INI


Tiba ya matatizo ya Ini hutegemea na chanzo chake,hivo kama una dalili hizi ongea na wataalam wa afya kwa ajili ya vipimo pamoja na Matibabu


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!