Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA MAWE KWENYE FIGO AU KIDNEY STONES(chanzo,dalili na Tiba)



 KIDNEY STONES

• • • • • •

UGONJWA WA MAWE KWENYE FIGO AU KIDNEY STONES(chanzo,dalili na Tiba)


Tatizo hili la mawe kwenye figo lina majina mengi kitaalam kama vile; kidney stones, Renal Calculi, Urolithiasis, Nephrolithiasis n.k je chanzo cha tatizo hili ni nini?


CHANZO CHA TATIZO HILI LA MAWE KWENYE FIGO


- tatizo hili huchangiwa na sababu nyingi mbali mbali kama vile;


• Mkojo kuwa na kiwango kikubwa cha Calcium, Oxalate na Uric acid kuliko kiwango cha maji kwenye Mkojo.


• Au mkojo kukosa vitu ambavyo vinazuia baadhi ya particles zilizopo kwenye mkojo kuungana kwa pamoja


Sababu zote hizi mbili husababisha madini pamoja na chumvi kuungana na kutengeneza vitu vigumu sana ndani ya Figo na ndipo tatizo hili hutokea(KIDNEY STONES)


BAADHI YA SABABU AMBAZO HUONGEZA UWEZEKANO WA KUTOKEA KWA TATIZO HILI


- Mtu kutokunywa maji ya kutosha kila siku


- Kuwa na mtu mwenye shida hii kwenye Familia


- Kula sana Baadhi ya vyakula ambavyo vina kiwango kikubwa sana cha Proteins, Sodium au chumvi pamoja na Sukari


- Tatizo la unene kupita kawaida


- Magonjwa ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula


- Mtu kufanyiwa upasuaji unaohusu figo au mfumo mzima wa chakula


- Matatizo mengine kama vile; Cystinuria, Hyperparathyroidism, uti inayojirudia mara kwa mara


- Matumizi ya Baadhi ya dawa  kwa muda mrefu kama vile; LAXATIVES n.k


DALILI ZA UGONJWA WA MAWE KWENYE FIGO NI PAMOJA NA;


✓ Kupata maumivu makali nyuma ya mbavu kwa ndani


✓ Kupata maumivu makali chini ya kitovu kuelekea kwenye via vya uzazi


✓ Kupata maumivu wakati wa kukojoa


✓ Kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa


✓ Kukojoa mkojo wenye rangi ya Pink, Brown au nyekundu


✓ kukojoa mara kwa mara


✓ kukojoa mkojo uliochanganyika na damu


✓ Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa


✓ Kupata kichefuchefu na kutapika


✓ Kukojoa mkojo wenye harufu kali


✓ Mkojo kutoka kwa shida sana

N.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


• Mara nyingi tatizo hili hupona baada ya mtu kunywa maji ya kutosha mfano lita 2.5 mpaka 3 kila siku endapo halijafikia hatua mbaya


• Lakini pia kuna dawa mbali mbali mgonjwa huweza kutumia kama vile;


 Dawa za maumivu mfano Ibuprofen, 


Dawa za kupitisha mawe yaliyobakia kwenye figo kama vile; Dawa jamii ya Alpha Blocker mfano FLOMAX(TAMSULOSIN) ambayo hufanya kazi ya kutanua njia ya mkojo na kusaidia mawe kupita kwa urahisi.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments