magonjwa
Ugonjwa wa SAFURA au Ugonjwa wa Minyoo dalili zake na Tiba yake
Ugonjwa wa Safura au minyoo (Hookworm Infection)
Maana ya Ugonjwa wa Safura
Safura ni neno ambalo hutumika kwa jamii nyingi lakini maana yake ni ugonjwa wa minyoo ya tumboni unaosababishwa na maambukizi ya minyoo aina ya hookworm (minyoo wenye umbo la ndoana) wanaoishi kwenye utumbo mdogo wa binadamu. Aina kuu zinazosababisha ugonjwa huu ni Necator americanus na Ancylostoma duodenale.
Minyoo hawa hujishikiza kwenye ukuta wa utumbo na kunyonya damu ya mtu, hivyo maambukizi makubwa yanaweza kusababisha pia tatizo la upungufu wa damu (anaemia).
Ugonjwa wa Safura ni ugonjwa ambao huwapata watu wengi hasa watoto wadogo.
CHANZO CHA UGONJWA WA SAFURA
– Ugonjwa wa Safura ni ugonjwa ambao husababishwa na Mashambulizi ya Minyoo aina ya HOOKWORMS
Jinsi Safura Inavyoambukizwa
Baadhi ya njia za maambukizi ya Ugonjwa huu ni;
1. Kupitia ngozi ya miguu
Njia kubwa ya maambukizi hutokea pale mtu anapotembea bila viatu kwenye udongo uliochafuliwa na kinyesi chenye mayai ya minyoo hawa. Mabuu ya minyoo hupenya kupitia ngozi na kuingia kwenye mwili.
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass,Kama unachangamoto yoyote ya kiafya;Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatSapp,Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaBaada ya kuingia mwilini:
- Huweza kusafiri kupitia damu hadi kwenye mapafu.
- Au hupanda kwenye koo.
- Au Mtu huyameza na kufikia utumbo mdogo ambako hukomaa na kuendelea kuzaliana.
2. Kumeza mayai ya minyoo
Pia Mtu anaweza kuambukizwa kwa kula chakula au kunywa maji yaliyochafuliwa na mayai ya minyoo.
Dalili za Ugonjwa wa Minyoo au Safura
Kumbuka Dalili hizi ni za jumla,hivo huweza kuingiliana na magonjwa mengine, pia Dalili hizi hutegemea kiwango cha maambukizi. Na Baadhi ya watu hawana dalili zozote lakini bado wana maambukizi haya,
DALILI ZA Jumla kwa UGONJWA WA SAFURA Ni pamoja na;
✓ Mtu kukosa hamu ya chakula
✓ Baadhi ya watu kula kupita kawaida
✓ Mwili kudhoofika ikiwa ni pamoja na kukonda sana
✓ Mwili kukosa nguvu kabsa
✓ Misuli ya mwili kuwa dhaifu
✓ Kupata maumivu ya tumbo mara kwa mara
✓ Mgonjwa kuharisha mara kwa mara
✓ Kuhisi dalili ya Minyoo njia ya haja kubwa wakati wa kujisaidia
✓ Pia baadhi ya wagonjwa hupata hali ya kikohozi ambacho hakiishi, Kuwashwa mwili n.k
NB: lakini maambukizi makubwa yanaweza kusababisha:
1.Upungufu wa damu (Anaemia)
Hii ndiyo athari kubwa zaidi kwa sababu minyoo hunyonya damu kwenye utumbo. Dalili zake ni pamoja na Uchovu wa mara kwa mara,Kizunguzungu,Kupumua kwa shida wakati wa kufanya kazi,Ngozi au macho kuwa na rangi ya kupauka(paleness) n.k.
2.Matatizo ya tumbo pamoja na mfumo wa mmeng’enyo chakula kwa ujumla
Mgonjwa anaweza kupata hali ya:
- Maumivu ya tumbo
- Kuharisha
- Kichefuchefu
- Kukosa hamu ya kula
3. Udumavu kwa watoto
Watoto wenye maambukizi ya muda mrefu wanaweza kupata tatizo la:Ukuaji hafifu wa mwili,Kupungua uwezo wa kujifunza,Udhaifu wa mwili kutokana na upungufu wa damu na virutubisho mwilini.
4. Dalili kwenye ngozi
Mahali ambapo mabuu huingia mwilini kunaweza kuwa na dalili kama vile: ngozi Kuwasha,vipele vidogo vidogo,Muwasho kwenye nyayo za miguu n.k
MATIBABU YA UGONJWA WA SAFURA
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Watu Walio Katika Hatari Zaidi
- Watoto wanaocheza kwenye udongo bila viatu
- Watu wanaoishi maeneo yenye usafi duni wa mazingira
- Wakulima wanaofanya kazi kwenye udongo bila kinga ya miguu au bila kuvaa viatu(peku)
- Watu wanaotumia vyoo visivyo salama au kujisaidia waziwazi n.k.
Vipimo vya Kugundua Safura au Minyoo
Uthibitisho wa ugonjwa hufanyika kwa:
- Kupima choo maabara (stool examination) ili kuona mayai ya minyoo.
Vipimo vya damu vinaweza pia kusaidia kuangalia kama kuna:
- Upungufu wa damu
- Mabadiliko yanayoweza kuendana na maambukizi ya vimelea n.k
Jinsi ya Kujikinga na Safura au maambukizi ya minyoo
1. Vaa viatu
Kuvaa viatu huzuia mabuu kupenya kwenye ngozi ya miguu,Usitembee peku.
2. Tumia vyoo vizuri
Epuka kujisaidia waziwazi kwa sababu kinyesi hueneza mayai ya minyoo kwenye mazingira.
3. Osha mikono vizuri
- Baada ya kutoka chooni
- Kabla ya kula au kuandaa chakula
4. Kuboresha usafi wa chakula na maji
Kula chakula kilichoandaliwa vizuri na kutumia maji salama pamoja na mazingira ya kupikia vyakula au kuandaa vyakula kuwa masafi sana.
5. Matibabu ya kinga katika maeneo yenye maambukizi mengi
Programu za afya ya jamii hutumia dawa za minyoo kupunguza maambukizi ya minyoo ya tumbo katika maeneo yenye tatizo kubwa.
References;
- World Health Organization (WHO). Soil-transmitted helminth infections (Hookworm, Roundworm and Whipworm).
https://www.who.int/health-topics/soil-transmitted-helminthiases - Centers for Disease Control and Prevention (CDC). Hookworm Infection – Biology and Treatment.
https://www.cdc.gov/parasites/hookworm/ - MSD Manual Consumer Version. Hookworm Infection (Ancylostomiasis).
- Wizara ya Afya Tanzania. Maelezo kuhusu Minyoo ya Tumbo na Kingatiba.
- Hesperian Health Guides. Minyoo – Safura (Hookworm).
- TUKI – Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Kamusi ya Kiswahili–Kiingereza: Safura (Hookworm disease).
Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa

