UPANDIKIZAJI WA Kinyesi au MAVI kwa Kitaalam Fecal/Poop transplant

 FAHAMU

• • • • • •

UPANDIKIZAJI WA Kinyesi au MAVI kwa Kitaalam Fecal/Poop transplant


Watu wengi tumezoea kusikia kuhusu upandikizaji wa Figo N.k Je umewahi kusikia hii ya upandikizaji wa kinyesi? soma hapa


Ukitajiwa unaweza kuhisi kinyaa, lakini kupandikizwa kinyesi 'mavi' (fecal/poop transplant) ni matibabu madhubuti kwa magonjwa makali (serious diseases). 


Upandikizwaji mavi (Fecal Transplant) ni kitendo cha kuchukua kinyesi cha mtu mwenye afya njema na kukiingiza katika utumbo mkubwa wa mtu mwenye maradhi. 


NANI ANAHITAJIKA KUPANDIKIZWA MAVI?


Upandikizaji huu hufanywa kwa mtu mwenye maambukizi makali ya bakteria aitwaye Clostridium Difficile, kifupi C.diff 


Kama ilivyo kwa maambukizi mengine ya bakteria,  C.diff hutibika kwa kutumia antibiotiki. Lakini kwa baadhi ya watu maambukizi haya huwa sugu na yenye kujirudia rudia kila mara. Hivyo, kuto itikia matibabu ya antibiotiki. 


Upandikizwaji mavi ni njia nzuri zaidi ya matibabu ya C.diff kwani huondoa maambukizi kwa uharaka zaidi. 


Kitendo hiki huingiza kinyesi chenye bacteria wazuri kwenye utumbo wako mkubwa. Hivyo, unapokuwa na bacteria wazuri wa kutosha kwenye utumbo mkubwa hupelekea kuwadhibiti wale bacteria wabaya wanaopelekea magonjwa kwenye utumbo. Hii ni faida tofauti na Antibiotiki ambazo huweza kuua bacteria wote wabaya na wazuri. 


UPANDIKIZAJI MAVI HUFANYWAJE?


Daktari  hukusanya kinyesi kutoka kwenye utumbo wa mtu mwenye afya na kukichanganya na maji ya saline, kisha kuchuja katika coffee filter. Matokeo huwa ni kimiminika chenye rangi ya kahawia (brown) ambacho huwa na bacteria wazuri. Kisha daktari huingiza kimiminika hicho ndani kwenye utumbo wa mgonjwa kwa kutumia bomba maalumu liitwalo colonoscope 


VIDONGE VYA KINYESI 'MAVI' (POOP CAPSULES)


Vidonge hivi havitumiki sana ila vipo na ndio njia mpya ya kufanya upandikizaji kinyesi. CHA KUSHUKURU VIDONGE HIVI HAVIMEZWI MDOMONI 😂. Daktari huviingiza ndani ya njia ya mmeng'enyo wa chakula kupitia tube inayopitishiwa puani mpaka tumboni. 


Vidonge hivi hutengenezwa kwa kupimwa kwanza kisha kuandaliwa na kugandishwa kwenye friji kisha kuwekwa ndani ya capsules (capsules ndio maganda ya kidonge mfano katika vidonge kama amoxicillin au doxycycline). Dozi yake utapatiwa vidonge 15 kwa siku 2 


Kinyesi kutoka kwa wachangiaji (Stool Donors) hutunzwa katika benki za vinyesi (Stool Banks) Cr:Dr.Tareeq




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!