FANGASI
• • • • • •
Watu ambao wapo kwenye Hatari ya kupata FANGASI wa mdomoni
Hii ni fangasi mdomoni na ulimi(oral candidiasis)
Hali hii husababishwa na kimelea aitwae C. albicans, C. glabrata, C. krusei na C. tropicalis.
Hali hii inawatokea watu wenye upungufu wa kinga mwilini na hata wasio na upungufu wa kinga
Walio kwenye hatari ya kupata fangasi hizi ni
1) Watu wenye kisukari
2)Watu wenye saratani ya damu
3)Watu wenye UKIMWI
4) Watu wanaotumia madawa ya antibiotiki kali na mara kwa mara na kwa muda mrefu
5) Watu wenye meno bandia
6)Watu wenye mdomo mkavu
7)Watu wenye magonjwa ya mafigo ,ini na moyo kufeli
8)Watu wanaopata matibabu ya saratani
9) Watu waliopandikiziwa viungo
Watu wengi wenye hali hii hua hawana dalili za kujionyesha; ugonjwa ukikolea mtu anaweza kupata dalili kama kuhisi mdomo mchungu,ulimi,mdomo kua na utando utando kama maziwa,maumivu ya fizi,midomo na hata kupata maumivu wakati wa kula au kumeza
TIBA
Hali hii inatibika vizuri sana; kama unahisi una hali hii nenda hospitali li uweze kutibiwa na upone kabisa
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!