MAUMIVU YA TUMBO
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA MAUMIVU YA TUMBO
Hizi hapa ni Baadhi ya Sababu ambazo zinaweza kuchangia maumivu ya Tumbo;
- Ugonjwa wa haja kubwa maarufu kama Irritable bowel syndrome (IBS)
- Ugonjwa wa kuvimba utumbo mpana maarufu kama Crohn au colitis
- Maumivu ya Tumbo wakati wa hedhi
- Kula Viambata vya Sumu kutoka kwenye chakula flani
- Tatizo la Allergy au Mzio juu ya aina flani ya chakula
- Tatizo la tumbo kujaa Gesi
- Maambukizi ya njia ya mkojo au UTI
- Shida ya misuli ya tumbo kuvuta
•Soma: dalili za Minyoo ya Ascariasis pamoja na Tiba yake
- Unaweza pia kupata maumivu ya tumbo ikiwa una tatizo la kukosa uvumilivu wa lactose mwilini
- au una tatizo la vidonda vya tumbo
- Ugonjwa wa maambukizi ya Bacteria kwenye via vya uzazi yaani PID
Sababu zingine ni pamoja na:
✓ Kuwa na tatizo la Hernia
✓ Kuwa na tatizo la Mawe kwenye figo yaani Kidney stones
✓ Tatizo la uvimbe kwenye kuta za ndani ya mji wa mimba yaani Endometriosis
✓ Kuwa na gastroesophageal reflux disease (GERD)
✓ Kuwa na tatizo la kuvimba kidole tumbo au appendix
✓ Kuwa na tatizo la Diverticulitis
✓ Kuwa na tatizo la Uvimbe kwenye mshipa mkubwa wa ateri tumboni yaani Aneurysm
✓ Tatizo la kuziba utumbo
✓ Saratani ya tumbo, kongosho, ini, mfereji wa nyongo, kifuko cha nyongo, au seli za kinga ya mwili
✓ Saratani ya ovary au tatizo la uvimbe kwenye vifuko vya mayai yaani ovarian cysts
✓ Pancreatitis (kuvimba kwa kongosho)
✓ Cholecystitis (kuvimba kwa kifuko cha nyongo)
✓ Mtiririko mdogo wa damu kwenye utumbo wako unaosababishwa na mishipa ya damu kuziba
✓ Tatizo la mimba kutunga Nje ya kizazi yaani Ectopic pregnancy
N.K
•Soma: dalili za Minyoo ya Ascariasis pamoja na Tiba yake
•Soma: Matibabu ya Ugonjwa wa Rheumatoid Arthritis
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!