DALILI ZA MINYOO JAMII YA ASCARIASIS

 MINYOO

• • • • •

DALILI ZA MINYOO JAMII YA ASCARIS

Ascariasis ni maambukizi ya Minyoo jamii ya ascaris lumbricoides, ambapo watu wengi huipata kwa kugusana na udongo ambao una minyoo hii mfano kwa watu wanaopenda kutembea peku au kutoka kwenye Maji

DALILI ZA MAAMBUKIZI YA MINYOO YA Ascaris lumbricoides

Tafiti zinaonyesha watu wengi wenye maambukizi ya Minyoo Ascariasis hawana dalili zozote,

Maambukizi ya kiwango cha wastani au makubwa husababisha ishara au dalili anuwai, kulingana na sehemu gani ya mwili wako imeathiriwa.

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili hizo kulingana na eneo husika;

 • Katika mapafu

 Baada ya kumeza mayai madogo (microscopic) ya ascariasis, huanguliwa kwenye utumbo mdogo na mabuu huhamia kupitia mfumo wa damu au mfumo wa limfu kwenye mapafu. 

 Katika hatua hii, unaweza kupata dalili sawa na pumu au nimonia, pamoja na:

 - Kikohozi cha kudumu

 - Kupumua kwa shida

 - Kutoa sauti wakati wa kupumua maarufu kama Wheezing sound

 Baada ya kutimia siku 10 hadi 14 kwenye mapafu, mabuu husafiri kwenda kooni

 • Katika Utumbo

 Mabuu hukomaa kuwa minyoo kwenye utumbo mdogo, na minyoo hiyo kwa kawaida hukaa ndani ya utumbo hadi kufa.  

Kwa mtu ambaye amepata maambukizi ya ascariasis ya wastani, huweza kupata uvimbe kwenye utumbo na unaweza kusababisha:

 - Maumivu madogo ya tumbo

 - Kichefuchefu na kutapika

- Kuhara kinyesi cha damu

 Ikiwa una idadi kubwa ya minyoo ndani ya utumbo, unaweza kuwa na:

 - Maumivu makali ya tumbo

- Uchovu wa mwili

 - Kichefuchefu na Kutapika

 - Kupungua kwa uzito wa mwili 

- au tatizo la utapiamlo

N.k

MATIBABU YA MINYOO YA Ascaris lumbricoides

Minyoo hii hutibiwa kwa dawa mbali mbali.

Na kwa maambukizi makubwa mgonjwa huweza kufanyiwa Upasuaji

•Soma: Madhara ya kubana Mkojo kwa Muda Mrefu

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!