Magonjwa
HALI YA KUHISI KUWASHWA SEHEMU MBALI MBALI MWILINI BAADA YA KUOGA
![](https://afyaclass.com/mk_omb/uploads/2021/07/images2B2528112529-1.jpeg)
AFYA TIPS
• • • • •
HALI YA KUHISI KUWASHWA SEHEMU MBALI MBALI MWILINI BAADA YA KUOGA
Hali ya kuhisi kuwashwa katika sehemu mbalimbali za mwili baada ya kuoga ni hali inayowapata wengi ila sio wote wanaofahamu chanzo chake.
Kulingana na wataalam wa ngozi sababu zifuatazo ndizo husababishwa mwasho baada ya kuoga.
Ukavu wa mwili au Xerosis hupata watu wa kila umri lakini huwa sana miongoni mwa wazee.
Hali hii hujitokeza pale ngozi yako inapokosa unyevu. Hii ni baada ya kuoga na maji moto au kutumia sabuni ambazo hukausha ngozi.
Ukavu wa ngozi pia unaweza kutokana na ukosefu wa vitamini A na B mwilini.
Sabuni unayotumia pia inaweza kuwa inachangia mwasho iwapo kemikali zilizotumiwa ni kali kwa ngozi yako.
•Soma:Faida na Hasara za Kuoga maji ya Baridi na maji ya Moto
Ili kukabiliana na hali hii wataalam wa ngozi wanashauri kuwa utumie loshoni itakayoweka unyevu kwenye ngozi yako muda mfupi tu baada ya kuoga. Usijifute na taulo bali jipake loshoni ukiwa bado upo na majimaji mwilini.
Vile vile unaweza kujaribu sabuni tofauti tofauti ili ubaini ni sabuni gani ambayo sio kali kwa mwili wako.
Ulaji wa mboga na matunda kwa wingi pia kutakusaidia kupata vitamini muhimu mwilini zitakazokusaidia kukabiliana na hali hii.
•Soma:Faida na Hasara za Kuoga maji ya Baridi na maji ya Moto
-
afyatips6 days ago
Faida za karafuu,Soma hapa kufahamu
-
Magonjwa4 days ago
Dalili za acid reflux,Soma hapa Kufahamu
-
magonjwa ya wanawake3 days ago
Dalili za Ectopic pregnancy,Mimba kutunga nje ya kizazi
-
Events6 days ago
Angalizo utoaji wa Dawa za Semaglutides,baada ya dawa bandia kuongezeka
-
Elimu&Ushauri2 days ago
Afya za watu bilioni 1.8 duniani matatani kwa kutokufanya Mazoezi – WHO
-
Events5 days ago
Mvulana mwenye Kifafa awa Wakwanza Duniani kuwekewa Kifaa kwenye Fuvu Lake
-
News5 days ago
Dola bilioni 1 kuwezesha uzalishaji wa chanjo Afrika
-
Events4 days ago
Princess Anne alilazwa hospitalini na majeraha madogo kufuatia tukio nyumbani kwake