BARIDI
• • • • •
Kipindi cha Baridi na Magonjwa mbali mbali(MAKALA YA LEO)
katika kipindi hiki cha Baridi magonjwa mengi hutokea kwa watu mbali mbali wa umri wote,Watoto,vijana na wazee,
Mbali na Magonjwa ambayo hutokea sana kipindi cha joto,pia Kuna magonjwa mengi sana hupenda kutokea kipindi cha baridi kama cha sasa hivi,
kipindi hiki cha sasa hivi watu hupatwa na magonjwa mbali mbali kama vile;
- Vikohozi ambavyo huambatana na Homa
- Mafua makali ya mara kwa mara
- Homa ya matumbo au ugonjwa wa Typhoid
- Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kwenye masikio, Koo n.k
- Hali ya kichefuchefu na kutapika mara kwa mara
- Mkusanyiko mkubwa wa nyongo ambao huweza kusababisha mvurugiko mkubwa wa tumbo pamoja na mwili mzima
- Ugonjwa wa Uti
- Ugonjwa wa Malaria huwapata sana Watu ambao wapo maeneo ya joto,ila hata kipindi cha Baridi unaweza pia kupata Malaria hivo jikinge
- Maumivu makali ya Viungo,mifupa na Misuli
- Tatizo la kizunguzungu kikali pamoja na maumivu makali ya Kichwa,kutokana na Watu wengi kutokunywa maji kipindi cha Baridi
N.k
Lakini pia kwa watu wenye vidonda mbali mbali,au matatizo kama ya Miguu n.k, hupata shida zaidi kwa kipindi hiki cha Baridi
MAMBO MUHIMU YAKUZINGATIA KATIKA KIPINDI HIKI;
- Tumia njia zote za kujikinga na Baridi ikiwa ni pamoja na;
✓ Kuvaa nguo nzito,masweta,Soks miguuni N.K
Kuna kiwango kikubwa cha Baridi hupenya kupitia Miguuni hivo Soks husaidia sana kukukinga na Baridi
✓ Epuka kushika Maji ya baridi mara kwa mara hasa wakati unafanya kazi kama vile; Kufua,Kupiga Deki,Kuoga N.k
✓ Hakikisha mtoto anafunikwa vizuri sana katika kipindi hiki cha Baridi
✓ Kama una dalili zozote za kuumwa,Nenda hospital kwa ajili ya Vipimo zaidi pamoja na matibabu yake
• Soma: Tatizo la kuota kinyama Ukeni
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!