MKOJO
• • • • •
MADHARA YA KUBANA MKOJO KWA MUDA MREFU MARA KWA MARA
Tunafahamu kwamba kuna Mazingira Mtu hubanwa na Mkojo halafu ni vigumu sana kupata huduma ya kujisaidia haja ndogo, Japo sio kila Mara.
Sasa endapo mtu anatabia ya Kubana Mkojo kila mara, hii ikiendelea kwa muda huweza kusababisha madhara makubwa kwa mhusika
HAYA HAPA NI BAADHI YA MADHARA YA KUBANA HAJA NDOGO KWA MUDA MREFU
- Kutanuka kwa Njia ya haja ndogo kuliko kawaida
- Kuwa katika hatari ya kupatwa na matatizo ya kibofu ikiwa ni pamoja na misuli ya kibofu kulegea
- Kuwa katika hatari ya kupata maambukizi kwenye mfumo wa haja ndogo yaani UTI
- Kupatwa na maumivu makali ya Tumbo chini ya kitovu
- Kuwa na tatizo la shinikizo la Damu
- Kibofu cha Mkojo kuanza kuvimba
- Mtu kuanza kuwashwa mwilini
- Miguu kuanza kuvimba mara kwa mara
N.K
HIVO UNASHAURIWA;
✓ kuepuka tabia ya kubana Mkojo mara kwa mara
✓ Nenda kajisaidie haja ndogo pale tu unapohisi uhitaji
✓ Kinga ni Bora kuliko Tiba
•Soma: Chanzo cha Tatizo la Kupata Choo kigumu na jinsi ya kupata Tiba
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!