MAMBO YAKUFANYA ILI KUSAIDIA DAWA IFANYE KAZI NA kuondoa Ukinzani wa Dawa(Drug Resistance)
DAWA
• • • • •
MAMBO YAKUFANYA ILI KUSAIDIA DAWA IFANYE KAZI NA kuondoa Ukinzani wa Dawa(Drug Resistance)
Jinsi ya Kuzuia Ukinzani wa Antibiotic au kwa kitaalam Drug resistance
Dawa kutokufanya kazi au Ukinzani wa dawa hutokea wakati bakteria wakitengeneza kinga dhidi ya dawa zilizoundwa ili kuwaua. Hii inafanya dawa kuwa haina maana dhidi ya aina mpya za vimelea sugu,
Ikiruhusu ukinzani kukua na kuenea kwa vijidudu vingine, na kutengeneza maambukizi yanayostahimili dawa ambayo inaweza kuwa ngumu kutibu.
Kinga ni njia bora ya kulinda dhidi ya ukinzani wa antibiotic. Kuna hatua nyingi ambazo watu wanaweza kuchukua ili kujilinda na familia zao kama vile:
1.Jifunze njia sahihi za kutumia dawa za kuua vimelea vya magonjwa kama vile Bacteria n.k
Sio maambukizi yote yanahitaji dawa. Lakini pia ongea na wataalam wa afya ili kuhakikisha unapata dawa sahihi ya kukinga au kutibu tatizo lako, kwa kipimo sahihi na kwa muda sahihi. Kamwe usitumie dawa za kukinga na magonjwa ikiwa mtaalamu wako wa huduma ya afya anasema hazihitajiki.
2. Epuka matumizi ya Dawa hovio
3. Epuka kukatisha matumizi ya dawa bila kumaliza Dose uliyopewa hata kama umepata nafuu au kupona kabsa
4. Kamwe Usitumie Antibiotic au dawa zilizobaki kwa muda mrefu,kuisha muda wa matumizi au zilizoexpire
5. Tumia dawa pale ambapo kuna ulazima wa kutumia dawa
ZINGATIA PIA BAADHI YA TIPS HIZI HAPA;
✓ Andaa Chakula safi na Salama
Chakula kama nyama, matunda, na mboga zinaweza kuchafuliwa na bakteria. Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) vinapendekeza hatua nne rahisi za kuandaa chakula salama nyumbani: Safi, kitenge, pika, na ubaridi.
✓ Kupata Chanjo
Ni muhimu sana kupata chanjo zote toka unazaliwa kwa magonjwa yote ambayo huzuiwa kwa chanjo kama vile; ugonjwa wa kupooza(polio),kifua kikuu,Surua N.k
✓ kunawa mikono yako
Miili yetu iko wazi kwa mamilioni ya viini vya magonjwa kama vile Bacteria,fangasi,virusi n.k. Kuosha mikono mara kwa mara kunaweza kusaidia kupambana na vijidudu na kuzuia magonjwa.
✓ Jua Dalili za magonjwa mbali mbali
Jifunze jinsi ya kutambua dalili za mapema za maambukizi ya magonjwa mbali mbali. Ikiwa unahisi una maambukizi au kuumwa, ongea na wataalam wa afya kwa ajili ya vipimo pamoja na matibabu.
✓ Uliza Maswali
Ongea na wataalam wa afya juu ya dawa za kukinga au kukutibu wanazokupa na ujifunze juu ya athari zinazoweza kutokea. Uliza juu ya kile wanachofanya na lengo kuu la kukupa dawa hizo ni nini
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!