UZAZI
• • • •
MWANAMKE KUBEBA MIMBA WAKATI NDYO AMETOKA KUJIFUNGUA
Watu wengi hawajui kwamba swala la mwanamke kubeba mimba mara baada ya kujifungua linawezekana, Mwisho wa siku wanakuja kubeba Mimba nyingine huku mtoto ni mdogo na bado ananyonya
FAHAMU; Uwezo wa Mwanamke Kubeba Mimba nyingine hutegemea kurudi kwa mzunguko wake wa Hedhi katika hali yake na Wala sio kusubiria Mpaka Mwanamke ablid au mtoto awe mkubwa,
Wapo wanawake wengi husubiria Kwanza Mpaka waone siku zao baada ya kujifungua,ndyo huanza kuchukua tahadhari za mimba zisizotarajiwa, bila kujua Blid ni matokeo ya yai ambao halikurutubishwa,
Hivo urutubishwaji ungetokea hata hiyo blid wanayoisubiria kwanza,wasingeweza kuiyona,Na ujauzito mwingine tayari wanao.
Soma: Kubeba Mimba nyingine huku una Mtoto mchanga ambaye bado ananyonya.
HIVO NI MUHIMU KUFAHAMU MAMBO HAYA YAFUATAYO;
1. Mwanamke anaweza kubeba Mimba nyingine baada ya Kujifungua kama mzunguko wake wa hedhi umekaa sawa na tayari mayai yameanza kupevushwa tena
2. Kumnyonyesha mtoto kunaweza kukusaidia usipate Mimba,japo sio kwa unyonyeshaji ambao wanawake wengi wanaufanya,
Hivo chukua tahadhari,usijidanganye kwamba unanyonyesha huwezi pata mimba
3. Blid ni matokeo ya yai kutokurutubishwa, Kama yai baada ya kutoka kwenye vifuko vyake halikurutubishwa na mbegu ya kiume ndipo blid hutokea,
hivo unaweza beba mimba hata kabla hujaona siku zako kwani kinachotangulia ni yai na baada ya yai kutokurutubishwa ndyo unapata blid
4. Chukua tahadhari kujikinga na Mimba ambazo hazijatarajiwa
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!