Sababu za upimaji wa ujauzito kwa kutumia ULTRASOUND

 UZAZI

• • • • •

Sababu za upimaji wa ujauzito kwa kutumia ULTRASOUND


 Ultrasound inaweza kutumika kwa sababu mbali mbali wakati wa ujauzito.  Daktari wako anaweza pia kuagiza uendelee kufanyiwa kipimo cha ultrasound zaidi ikiwa aligundua shida katika uchunguzi wa awali. 


Ultrasound inaweza pia kufanywa kwa sababu zisizo za kiafya, kama vile kutoa picha kwa wazazi au kuangalia jinsia ya mtoto.  Hata kama teknolojia ya ultrasound ni salama kwa mama na mtoto, wataalam wa afya hawashauri matumizi zaidi wakati hakuna sababu ya matibabu au faida.


 1. Kipimo cha Ultrasound kwenye miezi mitatu ya mwanzoni ya ujauzito yaani first trimester


 Katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito (wiki ya kwanza hadi ya 12), ULTRASOUND huweza kufanywa kwa ajili ya:


 - Kuthibitisha ujauzito


 - Kuangalia kama mtoto yupo hai


 - Kuangalia umri wa ujauzito wa mtoto na pamoja na tarehe ya matarajio ya kujifungua


 - Kuangalia au kuchunguza kondo la nyuma, vifuko vya mayai au ovari, na kizazi


 - kugundua ujauzito ambao umetunga nje ya kizazi yaani ectopic pregnancy 


- Kuangalia ukuaji wowote usiokuwa wa kawaida katika kijusi


•Soma: jinsi ya kuzuia kichefuchefu na kutapika pamoja na chanzo chake


 2. Wakati wa miezi mitatu ya pili yaani second trimester


 Katika trimester ya pili (wiki 12 hadi 24) na trimester ya tatu (wiki 24 hadi 40 au kuzaliwa), ultrasound inaweza kufanywa kwa ajili ya:


- Kuendelea kufuatilia ukuaji wa mtoto tumboni pamoja na mlalo wa mtoto kwenye wiki za mwishoni Kama vile;


*mtoto kutanguliza matako yaani breech presentation


* kuwa katika transverse


* Au kutanguliza kichwa yaani cephalic presentation


-Kuangalia jinsia ya mtoto


-Kuendelea kuthibitisha kwamba mtoto ni mmoja tumboni au ni zaidi ya mmoja


 - Kuendelea Kuangalia kondo la nyuma ili kujua kama kuna shida yoyote, kama vile placenta previa ( kondo la nyuma kushuka zaidi na kufunika mlango wa kizazi) au Placenta abruption(kondo la nyuma kujitenga na mji wa mimba kabla ya kujifungua)


 - Kuangalia uwepo wa ugonjwa wa Down syndrome (kawaida hufanywa kati ya wiki 13 na 14)


-Kuangalia uharibifu wowote kwa mtoto kama vile wa viungo au mtiririko wa damu


- kufuatilia kiwango cha maji ya uzazi yaani amniotic fluid


-Kuangalia kama mtoto anapata oksijeni ya kutosha


 - kugundua shida yoyote kwenye vifuko vya mayai(ovari) au kwenye kizazi, kama vile uvimbe wakati ujauzito


 -Kupima urefu wa kizazi


- kuongoza vipimo vingine, kama vile amniocentesis


- Kuendelea kuangalia kama bado mtoto yupo hai au amefia tumboni

N.K


•Soma: jinsi ya kuzuia kichefuchefu na kutapika pamoja na chanzo chake



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!