UKE
• • • •
TATIZO LA KULEGEA KWA UKE
Kulegea kwa uke ni moja ya mada inayowakuna sana wakina mama na wakina dada . Wengi hupendelea zaidi kuwa na uke uliobana ili kuwafurahisha wenza wao.
Kuna nadharia dhana potofu nyingi sana kuhusu suala la uke wengine huamini kwamba Uke unatakiwa kupoteza hali ya kutanuka na kusinyaa na kuwa mkubwa miaka yote.
Uke ni kiungo chenye lastiki maana yake kinaweza kunanuka ili kuruhusu kutoka mfano mtoto na vitu kuingia yani uume. Lakini haitachukua muda mrefu kwa uke kusinyaa na kurudi katika hali ya kawaida.
Uke hutanuka, kulegelea na kuongezeka ukubwa kiasi fulani kadiri umri unavoongezeka na unavozaa zaidi. Sasa endelea kusoma makala yetu hii ili ufahamu vyema uke wako pamoja na fikra potofu kuhusu uke.
Nataka nikwambie kulegea kwa uke ni dhana mbaya ambayo inatumika kuwadhalilisha wanawake, na inawatokea zaidi hasa pale wanapoachana na wanaume zao.
Wanaume hutumia hiki kama kigezo na silaha ya kuwadhalilisha wanawake kwamba wana uke mpana na wenye maji (bwawa) kitendo ambacho siyo kizuri.
Soma: Tatizo la Uke Kujamba,Chanzo,Dalili na Tiba
Dhana potofu ni kwamba mwanamke mwenye kulegea kwa uke amekutana kimapenzi na wanaume wengi. Ukweli ni kwamba haijalishi umekutana na wanaume wangapi uke ni lastiki unaweza kutanuka na kusinyaa na ukaendelea kuwa kwenye ubora wake kama kawaida
Je Inawezekana Kutibu Kulegea Kwa Uke?
Uke Uliokaza siyo Kitu cha Lazima Sana
Ni muhimu kufahamu kwamba kuwa na uke uliokaza sana inaweza kuashiria una tatizo la kiafya hasa pale unapoingiliwa na kupata maumivu makali pamoja na kwamba mwenza wako amekuandaa vizuri.
Mwili wa mwanamke unaposisimka misuli ya uke inalegea ili kuruhusu uume kupenya vizuri.
Kama misuli ya uke bado imekaza basi itakufanya upate maumivu makali sana na hutofurahia na kumaliza tendo la ndoa.
Kama tatizo la maumivu ya uke yataendelea basi weka apointment na dactari wa magonjwa ya wanawake ili upate vipimo na ushauri zaidi maana unaweza kuwa na matatizo yafuatayo;
- Hujaandaliwa vizuri na uke kutolowa inavotakiwa
Mwili wa mwanamke unaposisimuliwa basi huweza kutoa majimaji ya asili ambayo hulaishisha uke. Hivo hakikisha mwenza wako anakuaanda vizuri kabla ya kukuingilia. Kama una tatizo la kupata majimaji kidogo haijalishi umeandaliwa kiasi gani basi
- Maambukizi au ugonjwa kama vile kwenye via vya uzazi yaani PID,Fangasi,UTI n.k
Maambukizi hasa ya kupitia ngono ni chanzo cha kupata maumivu wakati wa tendo.
- Ajali na Msongo wa mawazo kupita kiasi.
Ajali kwenye maeneo ya nyonga na mfumo wa uzazi kwa ujumla inaweza kusababisha maumivu makali wakati watendo la ndoa na kukaza kwa uke. Hivo hakikisha umepona vizuri kabla hujaanza kushiriki ngono
- Tatizo la Viginismus
Vaginismus ni tatizo la uke ambapo misuli ya uke inaweza kukaza pasipo hiyari ya mwanamke na hio kuzuia uume kupenya. Wanawake wachache sana hukubwa na tatizo hili yaweza kuwa mmoja kati ya wanawake 500.
Tatizo hili linaweza kuletekezwa na hofu na msongo wa mawazo. dactari anaweza kutumia tiba zaidi ya moja katika kutatua shida hii ikiwemo kuongea na mgonjwa na kumshauri ama kutumia vifaa vya kutanua uke.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!