VITU VINAVYOCHANGIA MWANAMKE KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI

 VITU VINAVYOCHANGIA MWANAMKE KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI


➡️ Dr.Ombeni Mkumbwa



kumekuwa na Ongezeko kubwa la wanawake Kujifungua kwa Upasuaji hivi sasa.Hebu tuangalie baadhi ya sababu za tatizo hili


VITU VINAVYOCHANGIA MWANAMKE KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI NI PAMOJA NA;



~Mtoto kuwa mkubwa kuliko njia ya kupitia au Njia kuwa ndogo kiasi kwamba mtoto hawezi kupita.Kitaalam tunasema CEPHALOPELVIC DISPROPORTION(CPD)



~Njia kushindwa kufunguka ili mtoto apite wakati wa kujifungua


~Kondo la Nyuma kushuka na kufunika njia ya mtoto kupita,kitaalam hali hii inaitwa Placenta praevia


~Kondo la nyuma kuachia kabsa,sehemu lilipojishikiza,kitaalam tunasema Placenta abruption


~Ugonjwa wa Kifafa cha Mimba,ambapo njia salama ya tatizo hili ni mtoto azaliwe,hivo mama mwenye kifafa cha mimba anaweza kusaidiwa kwa kuzalishwa kwa Njia ya Upasuaji


~Mama mjamzito mwenywe kuomba afanyiwe upasuaji kwa sababu zake mwenyewe.


~Mama kuishiwa nguvu na kushindwa kusukuma mtoto


~Mtoto kukaa vibaya tumboni


~ Ujauzito wa kwanza kujifungua kwa Upasuaji, Mwanake huyu yupo kwenye asilimia kubwa hata Ujauzito mwingine kujifungua kwa Njia hyo hyo.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!