DAMU
• • • • • •
CHANZO CHA DAMU KUCHAFUKA
Hivi kuchafuka kwa Damu ni kitu gani?
Bila shaka umewahi kusikia au hata wewe menyewe umeshawahi kuambiwa una tatizo la damu kuchafuka baada ya kuwa na dalili flani za kuumwa, je kuchafuka kwa damu ni kitu gani? au ina maana gani mtu akisema damu imechafuka?
Kuchafuka kwa damu ni kiswahili ambacho hutumika sana ila tafsri yake ni "SEPSIS or Blood Infection" Kwa lugha ya kitaalam zaidi, huku tukiwa na maana ya maambukizi kwenye damu ambapo kinga ya mwili wako huanza kuzalisha kemikali wakati ikipambana na mashambulizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Bacteria N.k
Tatizo hili hutokea zaidi kwa watu wenye kinga ndogo ya mwili kama vile: Wenye tatizo la Saratani,maambukizi ya ukimwi, wanaotumia dawa ambazo huweza kuleta athari kwenye mfumo wa kinga ya mwili n.k
Tafiti zinaonyesha pia Wenye ugonjwa wa Kisukari, waliofanyiwa upasuaji, wazee pamoja na wajawazito hupatwa sana na tatizo hili.
DALILI ZA KUCHAFUKA KWA DAMU
Baada ya mtu kupatwa na maambukizi ya vimelea vya magonjwa mbali mbali kwenye damu kama vile Bacteria na kinga ya mwili kuanza kupambana na mashambulizi hayo ndipo mtu huanza kupata dalili mbali mbali kama vile;
- Mwili kuanza kutoa jasho jingi sana kuliko kawaida
- Ngozi ya mwili kubadilika rangi yake ya asili
- Mtu kuanza kupatwa na uchovu wa mwili kupita kawaida
- Mtu kuanza kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika mara kwa mara
- Kupatwa na maumivu makali ya kichwa
- Kupatwa na tatizo la kuharisha
- Mapigo yako ya moyo kuanza kubadilika na kwenda mbio mara kwa mara
- Kuanza kukojoa mkojo mdogo kuliko kawaida
- Joto la mwili kuwa juu sana au mgonjwa kuwa na homa
- Kuanza kuhisi baridi kali mwilini N.k
ENDAPO HUKUPATA TIBA YOYOTE NINI HUTOKEA?
• Endapo tatizo hili likawa la mda mrefu na mtu hakupata tiba huweza kuleta madhara makubwa mwilini kama vile;
1. Matatizo ya moyo
2. Matatizo ya Ubongo
3. Matatizo ya Mapafu
4. Tatizo la Figo kufeli N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!