CHANZO CHA MWANAMKE KUVUJA DAMU BAADA YA UJAUZITO KUTOKA NA JINSI YA KUZUIA

AFYA TIPS

• • • • • • •

CHANZO CHA MWANAMKE KUVUJA DAMU BAADA YA UJAUZITO KUTOKA NA JINSI YA KUZUIA


Mwanamke kuvuja damu baada ya mimba kutoka ni kawaida japo inategemea na wingi wa damu pamoja na muda ambao damu huendelea kutoka, wapo wanawake ambao hupata damu kidogo na ndani ya muda mfupi hukauka, na wapo wengine hupata madhara zaidi ambapo damu huendelea kutoka nyingi na kwa muda mrefu zaidi.


Katika makala hii tunachambua kuhusu wale ambao huvuja damu nyingi na kwa muda mrefu ambapo hili ni tatizo na wala sio kawaida.


SABABU ZA TATIZO HILI


Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili la mwanamke kuvuja damu nyingi na kwa muda mrefu baada ya ujauzito kutoka na sababu hizo ni kama vile;


- Tatizo la mji wa mimba kushindwa kusinyaa(contract) na kurudi kwenye hali ya kawaida ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Uterine atony


- Kubaki kwa baadhi ya mabaki ya ujauzito ndani ya mji wa mimba hali ambayo hupelekea mwanamke baada ya ujauzito kutoka kuendelea kuvuja damu nyingi


- Mji wa mimba kupata majeraha,kutoboka n.k


- Mwanamke kupata michubuko au vidonda kwenye shingo ya kizazi hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Cervical Laceration


- Mwanamke kupatwa na tatizo la damu kushindwa kuganda yaani Coagulopathy

N.k


MATIBABU


Licha ya kwamba Wanawake wengi wakiwa kwenye hali hii hutumia dawa mbali mbali ikiwemo za maumivu kama vile Ibuprofen, Unashauriwa kuonana na wataalam wa afya kwanza ili kujua chanzo cha hiyo blid ambayo haikati,ndipo matibabu yaanzie hapo.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!